CBC Grade 8 Kiswahili End Term 2 Exam 2026 · Question 4
(c) Taja na ueleze kipengele kimoja cha uwasilishaji kilichotumika katika hadithi hii. (Alama 2)
From Kiswahili — End of Term 2 Assessment 2026 (Set 9) · 2 marks · Topic: Fasihi, Uwasilishaji
ZOEZI II: FASIHI SIMULIZI (alama 15)
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Zamani za kale, kobe alikuwa mnyama aliyetembea haraka sana. Aliweza kukimbia hata zaidi ya swara na paa. Alijivunia sana na kuwakejeli wanyama wengine waliotembea polepole.
Siku moja, kobe alifanya shindano la mbio na simba. Wanyama wote walikusanyika kushuhudia. Kabla ya mbio kuanza, kobe alimtukana simba na kusema, “Simba, wewe ni mfalme wa msitu lakini huna kasi. Nitakufundisha adabu leo!”
Simba hakupendezwa na maneno hayo, lakini alijizuia na kusema, “Twende, tutakutana uwanjani.” Walipoanza kukimbia, kobe alikimbia sana hadi akaanguka kwa kishindo. Mguu wake ukavunjika na mgongo wake ukapasuka. Tangu siku hiyo, mgongo wake ukaonekana kuwa na mipasuko na akaacha kukimbia kabisa.
Wanyama walimcheka kobe, na tangu hapo akaamua kuwa mpole na kutembea taratibu ili asipate aibu tena.
(c) Taja na ueleze kipengele kimoja cha uwasilishaji kilichotumika katika hadithi hii. (Alama 2)
Answer
Mazungumzo (dayalojia): kobe na simba wanazungumzana, k.m. "Twende, tutakutana uwanjani."
Kipengele pamoja na mfano.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- (d) Tofautisha kati ya hadithi ya hurafa na ya hekaya (Alama 6)Question 5
- (e) Taja sifa tatu za hadithi za hekaya (Alama 3)Question 6
- (a) Andika anwani mwafaka kwa Novela hii. (Alama 1)Question 7
- (b) Taja mhusika mkuu katika Novela hii. (Alama 1)Question 8
- (c) Tambua na ueleze sifa nne za mhusika mkuu. (Alama 8)Question 9
- (a) Taja wahusika wawili katika tamthilia hili na ueleze uhusiano wao wa kifamilia. (Alama 2)Question 10