CBC Grade 8 Kiswahili End Term 2 Exam 2026 · Question 6
(e) Taja sifa tatu za hadithi za hekaya (Alama 3)
From Kiswahili — End of Term 2 Assessment 2026 (Set 9) · 3 marks · Topic: Fasihi, Hekaya
ZOEZI II: FASIHI SIMULIZI (alama 15)
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Zamani za kale, kobe alikuwa mnyama aliyetembea haraka sana. Aliweza kukimbia hata zaidi ya swara na paa. Alijivunia sana na kuwakejeli wanyama wengine waliotembea polepole.
Siku moja, kobe alifanya shindano la mbio na simba. Wanyama wote walikusanyika kushuhudia. Kabla ya mbio kuanza, kobe alimtukana simba na kusema, “Simba, wewe ni mfalme wa msitu lakini huna kasi. Nitakufundisha adabu leo!”
Simba hakupendezwa na maneno hayo, lakini alijizuia na kusema, “Twende, tutakutana uwanjani.” Walipoanza kukimbia, kobe alikimbia sana hadi akaanguka kwa kishindo. Mguu wake ukavunjika na mgongo wake ukapasuka. Tangu siku hiyo, mgongo wake ukaonekana kuwa na mipasuko na akaacha kukimbia kabisa.
Wanyama walimcheka kobe, na tangu hapo akaamua kuwa mpole na kutembea taratibu ili asipate aibu tena.
(e) Taja sifa tatu za hadithi za hekaya (Alama 3)
Answer
Mhusika mkuu ni mjanja; humshinda mwenye nguvu au mamlaka kwa akili; huchekesha.
Hekaya ni hadithi za ujanja.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- (a) Andika anwani mwafaka kwa Novela hii. (Alama 1)Question 7
- (b) Taja mhusika mkuu katika Novela hii. (Alama 1)Question 8
- (c) Tambua na ueleze sifa nne za mhusika mkuu. (Alama 8)Question 9
- (a) Taja wahusika wawili katika tamthilia hili na ueleze uhusiano wao wa kifamilia. (Alama 2)Question 10
- (b) Eleza jambo ambalo Amani anazungumzia kwa msisitizo katika mazungumzo haya. (Alama 2)Question 11
- (c) Jadili sifa mbili za Amani kama zinavyoonekana katika mazungumzo haya. (Alama 2)Question 12