CBC Grade 8 Kiswahili End Term 2 Exam 2026 · Question 5
(d) Tofautisha kati ya hadithi ya hurafa na ya hekaya (Alama 6)
From Kiswahili — End of Term 2 Assessment 2026 (Set 9) · 6 marks · Topic: Fasihi, Hurafa na Hekaya
ZOEZI II: FASIHI SIMULIZI (alama 15)
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Zamani za kale, kobe alikuwa mnyama aliyetembea haraka sana. Aliweza kukimbia hata zaidi ya swara na paa. Alijivunia sana na kuwakejeli wanyama wengine waliotembea polepole.
Siku moja, kobe alifanya shindano la mbio na simba. Wanyama wote walikusanyika kushuhudia. Kabla ya mbio kuanza, kobe alimtukana simba na kusema, “Simba, wewe ni mfalme wa msitu lakini huna kasi. Nitakufundisha adabu leo!”
Simba hakupendezwa na maneno hayo, lakini alijizuia na kusema, “Twende, tutakutana uwanjani.” Walipoanza kukimbia, kobe alikimbia sana hadi akaanguka kwa kishindo. Mguu wake ukavunjika na mgongo wake ukapasuka. Tangu siku hiyo, mgongo wake ukaonekana kuwa na mipasuko na akaacha kukimbia kabisa.
Wanyama walimcheka kobe, na tangu hapo akaamua kuwa mpole na kutembea taratibu ili asipate aibu tena.
| hadithi ya hurafa | hadithi ya hekaya |
|---|---|
(d) Tofautisha kati ya hadithi ya hurafa na ya hekaya (Alama 6)
Answer
1. Hurafa: wahusika ni wanyama tu – Hekaya: mhusika mkuu ni mjanja, binadamu au mnyama (k.m. Abunuwasi, Sungura). 2. Hurafa: hufundisha funzo kupitia tabia za wanyama – Hekaya: huonyesha mjanja akiwashinda wenye nguvu au mamlaka kwa akili. 3. Hurafa: mara nyingi huonya au hueleza chanzo cha jambo – Hekaya: hulenga kuchekesha kwa ujanja wa mhusika.
Linganisha wahusika, lengo na matukio.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- (e) Taja sifa tatu za hadithi za hekaya (Alama 3)Question 6
- (a) Andika anwani mwafaka kwa Novela hii. (Alama 1)Question 7
- (b) Taja mhusika mkuu katika Novela hii. (Alama 1)Question 8
- (c) Tambua na ueleze sifa nne za mhusika mkuu. (Alama 8)Question 9
- (a) Taja wahusika wawili katika tamthilia hili na ueleze uhusiano wao wa kifamilia. (Alama 2)Question 10
- (b) Eleza jambo ambalo Amani anazungumzia kwa msisitizo katika mazungumzo haya. (Alama 2)Question 11