naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili End Term 2 Exam 2026 · Question 3

(b) Eleza ujumbe mmoja unaopatikana katika hadithi hii. (Alama 2)

From Kiswahili — End of Term 2 Assessment 2026 (Set 9) · 2 marks · Topic: Fasihi, Ujumbe

ZOEZI II: FASIHI SIMULIZI (alama 15)
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Zamani za kale, kobe alikuwa mnyama aliyetembea haraka sana. Aliweza kukimbia hata zaidi ya swara na paa. Alijivunia sana na kuwakejeli wanyama wengine waliotembea polepole.
Siku moja, kobe alifanya shindano la mbio na simba. Wanyama wote walikusanyika kushuhudia. Kabla ya mbio kuanza, kobe alimtukana simba na kusema, “Simba, wewe ni mfalme wa msitu lakini huna kasi. Nitakufundisha adabu leo!”
Simba hakupendezwa na maneno hayo, lakini alijizuia na kusema, “Twende, tutakutana uwanjani.” Walipoanza kukimbia, kobe alikimbia sana hadi akaanguka kwa kishindo. Mguu wake ukavunjika na mgongo wake ukapasuka. Tangu siku hiyo, mgongo wake ukaonekana kuwa na mipasuko na akaacha kukimbia kabisa.
Wanyama walimcheka kobe, na tangu hapo akaamua kuwa mpole na kutembea taratibu ili asipate aibu tena.

(b) Eleza ujumbe mmoja unaopatikana katika hadithi hii. (Alama 2)

Answer

Kiburi na majivuno huleta aibu na hasara.

Kilichompata kobe.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test