naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 19

Kulingana na Zuhura ni nani anayeweza kufanikiwa?

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 3) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 14 hadi la 20.
Katika kijiji cha Maendeleo, kulikuwa na kijana mmoja aliyejulikana kwa jina Zuhura. Alikuwa fundi mchanga lakini hodari sana katika kutengeneza vifaa vya nyumbani kwa kutumia mbao. Alipoanza kazi, watu wengi walimdharau kwa kuwa alikuwa mchanga na hakuwa na duka kubwa la kisasa. Lakini kwa ustadi wake, kazi zake zilianza kuvutia wanakijiji na hata watu kutoka vijiji vya majirani.

Kazi ya mikono aliyokuwa akifanya ilikuwa ya kipekee. Kila kiti, meza au kabati aliyotengeneza ilikuwa imara na yenye muundo wa kuvutia. Alizingatia maadili ya kazi kama vile uaminifu, ubora na kuheshimu muda wa mteja. Watu waliokuwa wakishuku uwezo wake mwanzoni walibadilika na kuwa wateja wake wa kudumu. Hata shule ya msingi ya kijiji ilimwajiri kutengeneza madawati mapya.

Zuhura hakuwahi kuwa na kiburi bali alitumia mafanikio yake kuwashauri vijana wengine kuhusu umuhimu wa bidii na kujituma. Kwa sasa, yeye hufundisha vijana katika karakana ndogo aliyojenga mwenyewe akiamini kuwa kila mtu anaweza kufaulu maadamu ana nidhamu, subira na lengo maishani.

19. Kulingana na Zuhura ni nani anayeweza kufanikiwa?

  1. AVijana kutoka nyumba tajiri
  2. BMaskini wanaotia bidii
  3. CMtu yeyote bora ana bidii
  4. DMarafiki wanaotembea pamoja

Answer

C. Mtu yeyote bora ana bidii

"Kila mtu anaweza kufaulu maadamu ana nidhamu, subira na lengo."

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test