CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 11
Methali ifuatayo imetumiwa katika ufahamu isipokuwa
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali 8 hadi 14.
Duru za kuaminika siku hizi zinadai kuwa nyumba njema si mlango, fungua uingie ndani. Si hayo tu, pia inasemwa, nami naamini kuwa usikihukumu kitabu kwa jadala lake. Dunia rangi rangile. Imebadilika hasa katika ulimwengu wa jinsi ya lake hivi kwamba kile ukionacho sicho kilicho.
Sijui kama wewe umesikia kuhusu habari kwamba sehemu mbalimbali za mwili zinanunuliwa! si meno, si kope, si kucha, si nyonga, si nywele, si mboni.... kutaja zote ni muhali. Pengine waanzilishi walilenga kusaidia wale ambao kwa sababu moja au nyingine walipoteza sehemu hizo za mwili, au kufunikia hitilafu. Lakini madada zetu ni kina nani? Wameinukia juujuu kuonyesha kuwa japo jalali aliwaumba, hawakuumbika.
Hapa nilipo ninaafikiana na waliosema kuwa kazi ya Mungu haina makosa. Lakini kuwatajia madada zetu hilo ni sawa na kucheza ngoma goya, sisemi kupigia mbuzi gitaa lazima waige asili ya kizungu. Basi utawaona walivyojibebesha magunia ya nywele ama kwa kusukiwa au kubandikiwa. Nywele zenyewe ni nyeusi impasavyo mwafrika wa kawaida. La, sharti zitiwe nakshi kwa rangi ainati. Machoni napo wanatandaza kope hata kupepesa macho kwao ni kazi.
Wengine wasioridhika kuwa kizimwili, wanaodhani kuwa rangi ya kizungu ndiyo urembo hawajalishwi na madhara ya kumeza tembe - sumu ili kubadili rangi ya ngozi. Hata wapo wadungwao sindano ili kujiongezea uzani kupata kiuno cha nyigu na umbo la nane? Hawawazii madhara ya kudhuru mwili kwa kuuletea maradhi kama vile saratani.
11. Methali ifuatayo imetumiwa katika ufahamu isipokuwa
- Anyumba njema si mlango, fungua uingie ndani.
- Bkazi ya Mungu haina makosa.
- Cusikihukumu kitabu kwa jalada lake.
- Dmsichana mrembo hakosi kasoro.
Answer
D. msichana mrembo hakosi kasoro.
Methali A, B na C zimo katika ufahamu; D haimo.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Aghalabu msusi,Question 12
- Wanaobadilisha au kugeuza rangi za miliQuestion 13
- Kwa jumla mwandishi anadhihirisha tabia gani ya kina dada?Question 14
- Ni nini maana ya kupiga marufuku kama ilivyotumika katika kifunguQuestion 15
- Kulingana na aya ya kwanza ni kweli kusema kuwaQuestion 16
- Kulingana na kifungu hiki, miti hukatwa kwa sababu hizi zote isipokuwaQuestion 17