naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 13

Wanaobadilisha au kugeuza rangi za mili

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali 8 hadi 14.
Duru za kuaminika siku hizi zinadai kuwa nyumba njema si mlango, fungua uingie ndani. Si hayo tu, pia inasemwa, nami naamini kuwa usikihukumu kitabu kwa jadala lake. Dunia rangi rangile. Imebadilika hasa katika ulimwengu wa jinsi ya lake hivi kwamba kile ukionacho sicho kilicho.

Sijui kama wewe umesikia kuhusu habari kwamba sehemu mbalimbali za mwili zinanunuliwa! si meno, si kope, si kucha, si nyonga, si nywele, si mboni.... kutaja zote ni muhali. Pengine waanzilishi walilenga kusaidia wale ambao kwa sababu moja au nyingine walipoteza sehemu hizo za mwili, au kufunikia hitilafu. Lakini madada zetu ni kina nani? Wameinukia juujuu kuonyesha kuwa japo jalali aliwaumba, hawakuumbika.

Hapa nilipo ninaafikiana na waliosema kuwa kazi ya Mungu haina makosa. Lakini kuwatajia madada zetu hilo ni sawa na kucheza ngoma goya, sisemi kupigia mbuzi gitaa lazima waige asili ya kizungu. Basi utawaona walivyojibebesha magunia ya nywele ama kwa kusukiwa au kubandikiwa. Nywele zenyewe ni nyeusi impasavyo mwafrika wa kawaida. La, sharti zitiwe nakshi kwa rangi ainati. Machoni napo wanatandaza kope hata kupepesa macho kwao ni kazi.

Wengine wasioridhika kuwa kizimwili, wanaodhani kuwa rangi ya kizungu ndiyo urembo hawajalishwi na madhara ya kumeza tembe - sumu ili kubadili rangi ya ngozi. Hata wapo wadungwao sindano ili kujiongezea uzani kupata kiuno cha nyigu na umbo la nane? Hawawazii madhara ya kudhuru mwili kwa kuuletea maradhi kama vile saratani.

13. Wanaobadilisha au kugeuza rangi za mili

  1. Ahutumia vidonge pasipo kujali hatari zake.
  2. Bhufishwa na ugonjwa wa saratani.
  3. Chuwazia madhara yanayoletwa na dawa.
  4. Dhutumia sindano kubadili rangi ya ngozi.

Answer

A. hutumia vidonge pasipo kujali hatari zake.

"Hawajalishwi na madhara ya kumeza tembe - sumu ili kubadili rangi ya ngozi"; sindano ni za kuongeza uzani.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test