CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 16
Kulingana na aya ya kwanza ni kweli kusema kuwa
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 15 hadi 19.
Ingawa serikali ilipiga marufuku uchomaji makaa miaka iliyopita, jambo la ajabu ni kuwa matumizi ya makaa yanazidi kuongezeka kila mwaka. Takribani asilimia saba ya kawi inayotumiwa kila mwaka nchini, inatokana na miti.
Hata hivyo, kuna sababu nyingine zinazowafanya watu kukata miti na kuvuruga mazingira yetu. Matumizi ya mbao kuundia fanicha, ujenzi wa nyumba ni baadhi ya sababu zinazochangia ukataji miti. Sehemu ya ardhi yenye misitu aghalabu huwa na kiuchumi hufanya wakulima kuziingilia sehemu hizi kukata miti na kujitengea nafasi ya kilimo.
Inakisiwa kuwa zaidi ya tani milioni moja za makaa zinatumiwa kila mwaka nchini. Ingawa wakenya pia hutumia gesi na mafuta taa kwa bidhaa za petroli, kutokana na hali hii watu wengi mijini na mashambani wamelazimika kutumia kuni na makaa.
Serikali ilipopiga marufuku uchomaji wa makaa, maelfu ya watumiaji wa makaa hawakuelekezwa kwenye njia zingine mbadala ya kujipatia kawi. Hivyo basi biashara ya makaa iliendelea kinyume cha sheria hadi leo. Hata hivyo, habari njema ni kuwa huenda misitu yetu ikapata nafuu kwani wakenya wengi wameanza kukumbatia kawi ya jua.
16. Kulingana na aya ya kwanza ni kweli kusema kuwa
- Aserikali inashiriki katika uchomaji wa makaa.
- Bserikali imesema asilimia saba ya makaa ichomwe.
- Cutumizi wa makaa bado unaendelea.
- Duchomaji wa makaa umesitishwa kabisa.
Answer
C. utumizi wa makaa bado unaendelea.
"Matumizi ya makaa yanazidi kuongezeka kila mwaka."
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Kulingana na kifungu hiki, miti hukatwa kwa sababu hizi zote isipokuwaQuestion 17
- Wakulima huingilia misitu iliQuestion 18
- Kulingana na aya ya mwisho, ni jambo gani litafanya misitu ipate nafuu?Question 19
- Kulingana na kifungu, moyo una jukumu gani?Question 20
- Ni nini hufanyika tumboni na utumboni?Question 21
- Ni yapi matatu muhimu yaliyotajwa kwa ajili ya kutunza afaya?Question 22