CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 15
Ni nini maana ya kupiga marufuku kama ilivyotumika katika kifungu
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 15 hadi 19.
Ingawa serikali ilipiga marufuku uchomaji makaa miaka iliyopita, jambo la ajabu ni kuwa matumizi ya makaa yanazidi kuongezeka kila mwaka. Takribani asilimia saba ya kawi inayotumiwa kila mwaka nchini, inatokana na miti.
Hata hivyo, kuna sababu nyingine zinazowafanya watu kukata miti na kuvuruga mazingira yetu. Matumizi ya mbao kuundia fanicha, ujenzi wa nyumba ni baadhi ya sababu zinazochangia ukataji miti. Sehemu ya ardhi yenye misitu aghalabu huwa na kiuchumi hufanya wakulima kuziingilia sehemu hizi kukata miti na kujitengea nafasi ya kilimo.
Inakisiwa kuwa zaidi ya tani milioni moja za makaa zinatumiwa kila mwaka nchini. Ingawa wakenya pia hutumia gesi na mafuta taa kwa bidhaa za petroli, kutokana na hali hii watu wengi mijini na mashambani wamelazimika kutumia kuni na makaa.
Serikali ilipopiga marufuku uchomaji wa makaa, maelfu ya watumiaji wa makaa hawakuelekezwa kwenye njia zingine mbadala ya kujipatia kawi. Hivyo basi biashara ya makaa iliendelea kinyume cha sheria hadi leo. Hata hivyo, habari njema ni kuwa huenda misitu yetu ikapata nafuu kwani wakenya wengi wameanza kukumbatia kawi ya jua.
15. Ni nini maana ya kupiga marufuku kama ilivyotumika katika kifungu
- Akukubalia
- Bkukataa
- Ckuimarisha
- Dkuchapa
Answer
B. kukataa
Kupiga marufuku ni kukataza au kukataa jambo lisifanywe.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Kulingana na aya ya kwanza ni kweli kusema kuwaQuestion 16
- Kulingana na kifungu hiki, miti hukatwa kwa sababu hizi zote isipokuwaQuestion 17
- Wakulima huingilia misitu iliQuestion 18
- Kulingana na aya ya mwisho, ni jambo gani litafanya misitu ipate nafuu?Question 19
- Kulingana na kifungu, moyo una jukumu gani?Question 20
- Ni nini hufanyika tumboni na utumboni?Question 21