naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 18

Mwandishi ana ujumbe gani katika utunzi wa shairi hili? (alama 2)

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 3) · 2 marks · Topic: Fasihi, Ujumbe

ZOEZI LA V: USHAIRI (alama 5)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Ewe simu wanifanya mraibu,
sina dakika sekunde wala nukta,
umeteka nyara, muda wangu.

Ewe simu wanifanya mpweke,
sina rafiki sina jirani wala jamaa,
umenitenga katika dunia yangu.

Ewe simu nimekata shauri,
sitaki tena utumwa kunifunga ovyo
sasa nitajiondoa, nitajikomboa

17. Mwandishi ana ujumbe gani katika utunzi wa shairi hili? (alama 2)

Answer

Simu na vifaa vya kidijitali vinaweza kututeka, kutupotezea muda na kutufanya wapweke, hivyo tuvitumie kwa kiasi.

Simu imemfanyia nini mshairi?

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test