naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 5

Unafikiri iwapo mkutano wa dharura usingefanyika, ni jambo lipi lingefanyika? (alama 2)

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 3) · 2 marks · Topic: Fasihi, Maudhui

ZOEZI LA II: FASIHI SIMULIZI (Alama 10)
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali.
Hapo zamani katika msitu wa Taita paliishi wanyama wengi. Kati ya wanyama hao alikuwa kifaru. Kifaru alisifiwa sana na wanyama wengine kutokana na nguvu zake. Kila alipopita vijana kama nyani na ngiri walisimama na kumshangilia kwa jinsi walivyovutiwa na umbo lake. Jambo hili lilimtia kiburi kifaru akawa kila mara anajipitia kwa miondoko na maringo kama tausi.

Siku moja, kifaru aliona kile alichodhani kilikuwa jiwe barabarani, akanyanyua na kutupa kwa nguvu zake zote. Lo! kumbe alichodhani kuwa jiwe alikuwa mzee kobe. Kitendo hicho kilimwacha mzee kobe na majeraha mabaya. Gamba lake ambalo awali lilikuwa laini lilipasuka nyufa kila mahali.

Wanyama wengine walighadhabishwa na kitendo hicho. Walimwomba kifaru amtake radhi mzee kobe lakini juhudi zao ziliambulia patupu. Kifaru alishikilia kuwa mzee kobe ndiye mkosaji kwa kuwa hakumpisha njia kama walivyofanya wanyama wengine. Hapo mzozano ukaanza wanyama wakawa ushirikiano waliokuwa nao ulifika tamati. Baada ya kufanya kazi kwa umoja ikawa kila mmoja anavuta upande wake.

Pakazuka ukosefu wa chakula na maji, afya yao ikaanza kudhoofika kwa kukosa chakula. Furaha yao ikawa karaha. Palitokea ugomvi kati ya wanyama kwa kuwa upendo umoja na amani vilikosekana, wengi walikata tamaa kwa shida zilizowakodolea macho. Dhuluma nyingine za wanyama zilitokana na binadamu ambao badala ya kuwasaidia waliwawinda na kuwaua kwa ngozi na nyama yao.

Mambo yalipozidi unga mkutano wa dharura uliandaliwa kiongozi akiwa simba walijadiliana kuhusu dhiki ambazo ziliwakumba wanyama, binadamu alipewa jukumu la kuwa mlinzi mkuu wa wanyama kuangalia maslahi yao kama vile tiba, chakula, maji, isitoshe kulinda makazi yao ikiwa ni pamoja na misitu na mbuga zao, kuanzia siku hiyo wanyama waliishi kwa furaha bila shida na dhiki zilizowakumba hapo awali.

4. Unafikiri iwapo mkutano wa dharura usingefanyika, ni jambo lipi lingefanyika? (alama 2)

Answer

Wanyama wangeendelea kuangamia kwa ukosefu wa chakula na maji, na ugomvi kati yao ungeendelea.

Mkutano ulimaliza shida zipi?

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test