naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 10

Taja sifa za mama yake Katana. (alama 1)

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 3) · 1 mark · Topic: Fasihi, Wahusika

ZOEZI LA III: NOVELA (alama 10)
Soma sehemu ya novela ifuatayo kisha ujibu maswali.
Katana alilelewa katika familia iliyoamini katika thamani ya kazi na juhudi za mtu binafsi. Mama yake alimuonya kila mara kuwa utajiri na mafanikio hayaji kwa bahati nasibu bali yanahitaji kukata jasho. Alikuwa amekulia kwenye maadili ya kujitegemea jambo ambalo lilimfanya awe na msimamo thabiti tangu umri mdogo. Hata katika umaskini wao, Katana hakuwahi kuona hali hiyo kama kisingizio cha kukata tamaa. Aliamini kuwa kila mtu ana uwezo wa kubadilisha maisha yake kama atafanya kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu ya fedha. Baada ya dhiki faraja.

Mara nyingi ungempata Katana akihangaika na vibarua kijijini akibeba mizigo kwenye soko au akifanya kazi za ujenzi. Hakuchagua kazi ilimradi inampa nafasi ya kupata pesa za kuweka akiba. Tofauti na vijana wenzake waliokuwa wakipoteza muda kwenye mabaraza, Katana alitumia kila dakika yake kujipatia chochote. Alikuwa na ndoto ya kumiliki biashara yake na hii ilimpa ari na nguvu za kifaru.

"Kila shilingi ina thamani," alijiambia kimoyomoyo kila mara alipoweka akiba yake kidogo kwenye akaunti yake ya benki. Hakutaka hata senti moja itumike kwa anasa au mambo yasiyo ya lazima. Alijua fika kuwa safari ndefu huanza kwa hatua.

Watu wa kijiji walimuona Katana kama mfano wa kuigwa, ingawa baadhi yao walimcheka kwa jitihada zake za kujinyima raha. Waliamini kuwa kijana anapaswa kufurahia maisha yake bila kujinyima.

9. Taja sifa za mama yake Katana. (alama 1)

Answer

Ni mshauri: alimuonya kuwa mafanikio yanahitaji kukata jasho.

Mama alimwambia nini Katana?

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test