CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 13
Andika sifa tatu za tamthilia. (alama 3)
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 3) · 3 marks · Topic: Fasihi, Sifa za Tamthilia
ZOEZI LA IV: TAMTHILIA (alama 10)
Soma sehemu ifuatayo ya tamthilia kisha ujibu maswali.
(Msituni Nyati na Sungura wanaishi pamoja kando ya mto mkubwa. Wote ni marafiki wa dhati. Sungura ana bidii kazini lakini mara kwa mara hujihisi kama hafai kwa kuwa ni mdogo sana akijilinganisha na Nyati)
Sungura: Nyati ndugu yangu ninaona mvua inaendelea kunyesha na karibu maji yatasomba daraja letu.
Nyati: Ni kweli lakini hata daraja likisombwa halitatuzuia kwenda katika shamba letu upande ule mwingine.
Sungura: (Kwa mshtuko) Vipi?
Nyati: Tutavuka kwa kuogelea.
Sungura: (Anaonekana kuhuzunika) Mimi sina uwezo wa kuogelea. Nina hofu sitaweza kupata chakula.
Nyati: Usijali ndugu yangu. Nitaogelea kisha nitafute chakula nilete nyumbani.
Sungura: Asante ndugu yangu (Siku iliyofuata daraja lilikuwa limefunikwa na maji. Nyati anaogelea na kuuvuka mto. Sungura anabaki nyumbani. Anahuzunika sana kwa kuwa Nyati amekawia sana kurejea nyumbani.)
Sungura: Mbona amekawia hivi? Nitaendelea kubaki nyumbani hadi lini (anamuona Nyati kwa mbali na kufurahia).
Nyati: (Baada ya kuvuka mto) Ndugu yangu mbona umehuzunika sana. Ilikuwa vigumu kupata chakula kwa kuwa mvua kubwa umeharibu mazao.
Sungura: (Analia) Nita...kaa hivi hadi lini? Sifai... sifai kabisa kuwa duniani. Nina mwili mdogo ila siwezi kuogelea. Wewe ni mkubwa na unaweza kuogelea.
Nyati: (Anamkaribia na kumpapasa mgongoni.) Usilie tena kaka. Kesho nitakubeba mgongoni kisha tuogelee pamoja. Tutaenda pamoja shambani. Kumbuka kila mmoja ameumbwa kwa uwezo tofauti. Ninaweza hili nawe unaweza lingine. Jithamini ndugu yangu kwa uwezo ambao Mungu amekupa. Wewe ni wa maana.
12. Andika sifa tatu za tamthilia. (alama 3)
Answer
Huwasilishwa kwa mazungumzo (dayolojia), huigizwa jukwaani, na majina ya wahusika huandikwa pembeni.
Angalia jinsi sehemu hii imeandikwa.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Je, mandhari ya tamthilia hii ni gani? (alama 2)Question 14
- Dhamira ya mwandishi wa tamthilia hii ni gani? (alama 3)Question 15
- Je, shairi hili lina beti ngapi? (alama 1)Question 16
- Shairi lina mishororo mitatu kwenye kila ubeti kwa hivyo ni shairi la ___ (alama 1)Question 17
- Mwandishi ana ujumbe gani katika utunzi wa shairi hili? (alama 2)Question 18
- Lipe shairi ulilosoma anwani. (alama 1)Question 19