naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 3 · Question 11

Kwa mujibu wa kifungu hiki, Mwewe:

From Kiswahili Karatasi ya 1 · 1 mark · Topic: Kusoma na Matumizi ya Lugha, Ufahamu na Sarufi

Urafiki wa kuku na mwewe ulikuwa wa kufa kuzikana. Waliishi kwa ushirikiano wa ulimi na mate. Walifanya shughuli zote pamoja. Walijua kuwa ndugu ni kufaana si kufanana. Walifaana kwa la jua na la mvua. Hali ya mmoja ingemwathiri mwenzake. Hawakukubali kamwe yeyote kuleta mzozo ambao ungeutia usuhuba wao ufa.
Hali hii ilibadilika pindi tu walipoanza kulea vifaranga. Kutokana na ulezi, Mwewe ndiye aliyekuwa akitafuta chakula kwa siku hiyo, kinyume na hapo awali ambapo walishirikiana katika shughuli zao.
Siku nyingine Kuku angewaacha vifaranga na kumpiga jeki rafikiye. Siku moja Mwewe alipokuwa akihitaji wembe, bila kusita Kuku alimpa wembe na kumsadia.
Katika harakati hizo, wembe uliteleza ukamkata mtoto wa Mwewe. Kuku alijaribu kumpa huduma ya kwanza lakini damu ilizidi kutiririka. Kuku akashikwa na wahaka, akajaribu kuomba usaidizi wa majirani lakini wakampuuza. Kumbe walikuwa wakingoja sana siku hii. Walilulia sana kuvunjika kwa usuhuba wa Kuku na Mwewe.
Mwewe alipofika jioni hiyo, majirani walimkimbilia na kumpasha habari Mwewe. Habari zenyewe zilitiliwa chumvi. Mwewe akapandwa na mori na kuanza vita. Rai za Kuku za kumtaka amsikilize kwanza hazikuzaa matunda. Urafiki wao wa miaka na mikaka ukafikia ukingoni.

Kwa mujibu wa kifungu hiki, Mwewe:

  1. AAlichoshwa kutafutia Kuku chakula.
  2. BAlikasirishwa na kujeruhiwa kwa mwanawe.
  3. CAlimsaidia Kuku kila wakati.
  4. DAlikuwa mwaminifu kwa Kuku.

Answer

B. Alikasirishwa na kujeruhiwa kwa mwanawe.

Jibu sahihi ni: Alikasirishwa na kujeruhiwa kwa mwanawe.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test