CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 3 · Question 16
Yafuatayo ni manufaa ya wenye mahitaji maalum kukaa mbele isipokuwa:
From Kiswahili Karatasi ya 1 · 1 mark · Topic: Kusoma na Matumizi ya Lugha, Ufahamu na Sarufi
Mwili wa binadamu umeundwa na viungo mbalimbali. Ikiwa moja kati ya viungo hivyo itashindwa kufanya kazi, vingine vitaathiriwa. Ni jambo la busara kila mtu kutunza viungo vyake ili shughuli za viungo hivyo ziendelee kufanyika ipasavyo.
Hata hivyo, kunao walio na ulemavu mbalimbali ambao wengi hutekeleza shughuli zao ipasavyo. Ajabu ni kuwa kunao wasiokuwa na ulemavu wowote ambao wamejikalia shambiro. Vilevile kunao wengi ambao wana mahitaji maalum katika jamii zetu. Yawezekana mahitaji haya si ulemavu tu, kuna mengine kama vile zeruzeru ambao huwa na matatizo ya macho. Huvaa miwani ili kupunguza mwangaza.
Basi wakiwa darasani, ni vyema mwalimu awapange kuketi mbele ya darasa karibu na ubao pasipo mwangaza mwingi. Vilevile wapo wanafunzi wasiosikia vizuri au kuona ipasavyo. Kundi hili pia lahitaji kuwekwa kuketi mbele ya darasa. Hali hii itawawezesha kushiriki na wenzao ipasavyo katika masomo. Pia mtagusano kati yao utajengeka vilivyo.
Sote tuwakubali namna walivyo na kuwapiga jeki wanapohitaji msaada wetu. Tunaposhirikiana nao katika shughuli mbalimbali, wao hujiamini na kutekeleza shughuli zao kikamilifu.

- AKuweza kuona maandishi vizuri.
- BKuweza kusikia vizuri mwalimu azungumzapo.
- CKuwatenga na wenzao ili wasishirikiane.
- DKuwawezesha kushiriki ipasavyo katika shughuli za kimasomo.
Answer
C. Kuwatenga na wenzao ili wasishirikiane.
Jibu sahihi ni: Kuwatenga na wenzao ili wasishirikiane.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Maana ya neno “mtagusano” kulingana na kifungu ni:Question 17
- Ni mwanafunzi gani anayependa ugali na chapati pekee?Question 18
- Ni vyakula vipi viwili vilivyopendwa mara nyingi zaidi kwa idadi sawa?Question 19
- Ni siku gani ambapo wanafunzi wote walipendelea vyakula tofauti?Question 20
- Ni salamu gani inayofaa wakati wa asubuhi uliotajwa katika mazungumzo?Question 21
- Chagua nahau sahihi kukamilisha nafasi ya 22 iliyoachwa kwenye kifungu.Question 22