CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 3 · Question 10
Aya ya pili imebainisha kwamba:
From Kiswahili Karatasi ya 1 · 1 mark · Topic: Kusoma na Matumizi ya Lugha, Ufahamu na Sarufi
Urafiki wa kuku na mwewe ulikuwa wa kufa kuzikana. Waliishi kwa ushirikiano wa ulimi na mate. Walifanya shughuli zote pamoja. Walijua kuwa ndugu ni kufaana si kufanana. Walifaana kwa la jua na la mvua. Hali ya mmoja ingemwathiri mwenzake. Hawakukubali kamwe yeyote kuleta mzozo ambao ungeutia usuhuba wao ufa.
Hali hii ilibadilika pindi tu walipoanza kulea vifaranga. Kutokana na ulezi, Mwewe ndiye aliyekuwa akitafuta chakula kwa siku hiyo, kinyume na hapo awali ambapo walishirikiana katika shughuli zao.
Siku nyingine Kuku angewaacha vifaranga na kumpiga jeki rafikiye. Siku moja Mwewe alipokuwa akihitaji wembe, bila kusita Kuku alimpa wembe na kumsadia.
Katika harakati hizo, wembe uliteleza ukamkata mtoto wa Mwewe. Kuku alijaribu kumpa huduma ya kwanza lakini damu ilizidi kutiririka. Kuku akashikwa na wahaka, akajaribu kuomba usaidizi wa majirani lakini wakampuuza. Kumbe walikuwa wakingoja sana siku hii. Walilulia sana kuvunjika kwa usuhuba wa Kuku na Mwewe.
Mwewe alipofika jioni hiyo, majirani walimkimbilia na kumpasha habari Mwewe. Habari zenyewe zilitiliwa chumvi. Mwewe akapandwa na mori na kuanza vita. Rai za Kuku za kumtaka amsikilize kwanza hazikuzaa matunda. Urafiki wao wa miaka na mikaka ukafikia ukingoni.

- AMajukumu ya ulezi yalifanya Kuku na Mwewe kufanya kazi kwa mpango.
- BMalezi ya vifaranga yalipunguza juhudi za Kuku kutafuta chakula.
- CHaikuwa kawaida ya Kuku kutafuta chakula.
- DJambo la kushangaza kuachwa kwa vifaranga lilikuwa ishara ya utengano.
Answer
B. Malezi ya vifaranga yalipunguza juhudi za Kuku kutafuta chakula.
Jibu sahihi ni: Malezi ya vifaranga yalipunguza juhudi za Kuku kutafuta chakula.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Kwa mujibu wa kifungu hiki, Mwewe:Question 11
- Ni funzo gani kuhusu ushawishi wa majirani linalotokana na kifungu hiki?Question 12
- Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza.Question 13
- Kulingana na kifungu hiki, ni kweli kuwa:Question 14
- Maana ya nahau “wamejikalia shambiro” ni kukaa:Question 15
- Yafuatayo ni manufaa ya wenye mahitaji maalum kukaa mbele isipokuwa:Question 16