naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 3 · Question 13

Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza.

From Kiswahili Karatasi ya 1 · 1 mark · Topic: Kusoma na Matumizi ya Lugha, Ufahamu na Sarufi

Mwili wa binadamu umeundwa na viungo mbalimbali. Ikiwa moja kati ya viungo hivyo itashindwa kufanya kazi, vingine vitaathiriwa. Ni jambo la busara kila mtu kutunza viungo vyake ili shughuli za viungo hivyo ziendelee kufanyika ipasavyo.
Hata hivyo, kunao walio na ulemavu mbalimbali ambao wengi hutekeleza shughuli zao ipasavyo. Ajabu ni kuwa kunao wasiokuwa na ulemavu wowote ambao wamejikalia shambiro. Vilevile kunao wengi ambao wana mahitaji maalum katika jamii zetu. Yawezekana mahitaji haya si ulemavu tu, kuna mengine kama vile zeruzeru ambao huwa na matatizo ya macho. Huvaa miwani ili kupunguza mwangaza.
Basi wakiwa darasani, ni vyema mwalimu awapange kuketi mbele ya darasa karibu na ubao pasipo mwangaza mwingi. Vilevile wapo wanafunzi wasiosikia vizuri au kuona ipasavyo. Kundi hili pia lahitaji kuwekwa kuketi mbele ya darasa. Hali hii itawawezesha kushiriki na wenzao ipasavyo katika masomo. Pia mtagusano kati yao utajengeka vilivyo.
Sote tuwakubali namna walivyo na kuwapiga jeki wanapohitaji msaada wetu. Tunaposhirikiana nao katika shughuli mbalimbali, wao hujiamini na kutekeleza shughuli zao kikamilifu.

Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza.

  1. AViungo hushindwa kutegemeana kwa sababu ya ukosefu wa ushirikiano.
  2. BUshirika ni msingi imara wa utendakazi.
  3. CViungo haviwezi kufanya kazi pamoja.
  4. DShughuli huathiriwa tukishindwa umuhimu wa kudhibiti kazi.

Answer

B. Ushirika ni msingi imara wa utendakazi.

Jibu sahihi ni: Ushirika ni msingi imara wa utendakazi.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test