CBC Grade 7 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 29
(c) Andika kibwagizo cha shairi hili. (alama 2)
From Kiswahili — End Term One Assessment 2025 (Set 6) · 2 marks · Topic: Fasihi, Ushairi
SEHEMU 4: FASIHI - SHAIRI
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
Fikiri zako fikira, ufikiri kila tendo,
Fikiri lilo na dhara, ufikiri na la pendo,
Fikiri lilo tohara, ufikiri na uvundo,
Fikiri fikiri tendo, la amani na busara.
Fikiri sana dunia, ina mzuri mdundo,
Fikiri sana yalia, ina mzuri mshindo,
Fikiri mwisho sikia, unapasuka msondo,
Fikiri fikiri tendo, la amani na busara.
Fikiri ndugu dahari, dunia ina mikondo,
Fikiri hizi habari, ni kushuka na mipando,
Fikiri dunia pori, chaka la uwi na kondo,
Fikiri fikiri tendo, la amani na busara.
Fikiri dau muundi, muunda dau muundo,
Fikiri lende kilindi, daule likaze mwendo,
Fikiri dau halendi, nguvu za dau upondo,
Fikiri fikiri tendo, la amani na busara.
(c) Andika kibwagizo cha shairi hili. (alama 2)
Answer
Fikiri fikiri tendo, la amani na busara.
Mstari unaorudiwa.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- (d) Shairi hili linazungumzia nini? (alama 2)Question 30
- (a) Pendekeza kichwa kinachofaa habari hii (alama 1)Question 31
- (b) Kuna tofauti gani kati ya adhabu na nidhamu? (alama 3)Question 32
- (c) Kulingana na hadithi, taja njia mbili za adhabu (alama 2)Question 33
- (d) Andika methali moja inayoambatana na hadithi hii? (alama 2)Question 34
- Makala haya yanazungumzia juu ya nini? (alama 1)Question 1