naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 1

Makala haya yanazungumzia juu ya nini? (alama 1)

From Kiswahili — End Term One Assessment 2025 (Set 6) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

KUSOMA UFAHAMU NA UFUPISHO
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yatakayofuata.
Kila sehemu ya nchi kuna miti. Miti ina faida nyingi. Si kwa binadamu tu bali hata kwa wanyama, ndege, wadudu na viumbe wa baharini. Kuna miti inayotoa vyakula kwa watu na kwa wanyama. Miti hiyo ni kama michungwa, mipapai, milimau, mipera, mikwanju, miwa, fito na kadhalika. Miti mingine hutupatia vifaa vya kukidhi mahitaji yetu. Vifaa hivyo ni kama samani yaani meza, makabati, viti, madawati na vifaa vingine kama vinu, michi, mipini ya majembe na mashoka, mivure na kadhalika. Miti hiyo ni kama mivule, mikalitusi, misonobari na mikangazi. Baadhi ya miti hutupa dawa za kutibu magonjwa mbalimbali. Halikadhalika, miti hutupa mvua na kutuepusha na jangwa. Miti pia hutupatia kuni na makaa ya kupikia vyakula. Miti hutumiwa kujengea mapaa ya nyumba. Vilevile, miti ni mapambo ya mazingira.
Kwa kuona faida na umuhimu wa miti, watu duniani wametenga siku maalum, kila mwaka, ya kupanda miti. Nchi yetu nayo haijabaki nyuma kama mkia bali nayo hushiriki kikamilifu katika shughuli ya upanzi wa miti. Mbali na siku hiyo maalum, serikali yetu inahamasisha raia kupanda miti. Jambo hili, hufanyika katika hafla mbalimbali. Walinda mazingira husema "Ukikata mti mmoja panda miwili."
Isitoshe, serikali ya Kenya imetunga sheria za kuzuia uharibifu wa misitu. Uharibifu huu unahusiana na ukataji wa miti kwa kutafuta kuni, kuchoma makaa na hata kuchoma misitu na vichaka ukitafuta malisho ya mifugo. Ikumbukwe kuwa misitu ni makazi ya ndege na wanyama wa porini. Misitu hii ikiharibika kutokana na ukataji wa miti, ndege na wanyama hawa watakosa vyakula na mahali pa kuishi. Miti ikiendelea kukatwa ovyo bila ya kupanda mingine ama misitu ikiendela kuharibiwa, mazingira yetu hayatakuwa safi. Nchi yetu Itakosa mvua na hata dunia nzima itageuka jangwa. Ni wajibu wetu kulinda mazingira kwa kupanda miti na kutoikata ovyo!

1. Makala haya yanazungumzia juu ya nini? (alama 1)

Answer

Umuhimu wa miti na utunzaji wake.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test