CBC Grade 7 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 7
Mwandishi alikusudia nini aliposema, 'umoja ni nguvu?' (alama 2)
From Kiswahili — End Term One Assessment 2025 (Set 6) · 2 marks · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yatakayofuata.
Mkurugenzi wa masomo, mkuu wa nidhamu, walimu na wanafunzi wote, hamjambo? Tumekutana sote hivi leo, viongozi, walimu na wanafunzi wa shule yetu ya Namundera ili tuzungumzie waziwazi juu ya umuhimu wa ushirikiano baina yetu sote iwapo tunataka maendeleo mazuri ya shule yetu.
Wahenga walisema: "Ngozi ivute ingali mbichi". Tupo mwanzoni mwa mwaka. Ndiyo maana nimewaita hapa ili tuanze safari ya mwaka huu. Hii ni safari ndefu na ngumu na msafiri ni aliye bandarini. Madhumuni ya kuwataka viongozi, walimu na wanafunzi kushirikiana ni kwa sababu matokeo mazuri yanategemea ushirikiano wetu sisi sote pamoja. Jifya moja haliinjiki chungu. Kitu ambacho ningependa kusisitiza ni kwamba wanafunzi wote ni sawa. Wawe wavulana, wawe wasichana. Hatuwezi kusema wanafunzi wa aina fulani huzaliwa wajinga na wengine wa aina nyingine huzaliwa werevu.
Mungu hakupanga hivyo kwani hana moyo wa kupendelea jinsia hii wala kuonea jinsia nyingine. Suala tunalokumbana nalo ni hili: Kwa nini shule fulani tu ndizo zenye matokeo na maendeleo mazuri kila kukicha? Ukaona kuwa wanafunzi wao hushinda vizuri, shule ina usafi na mengineyo. Jibu ni kwamba wanafunzi wote wa shule hizo huungana pamoja, wavulana kwa wasichana. "Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu." Kwa upande wa masomo, wanafunzi nawakumbusha kwamba, "Mtaka cha mvunguni sharti ainame." Matokeo mazuri yatatokana na ustahimilivu, jitihada, mshikamano na kujitolea. Wenzenu kutoka shule nyingine ndivyo wafanyavyo. Nawashukuru kwa kunisikiliza na ninadhani kuwa maneno yangu hayajapita sikio hadi sikio. Asanteni
7. Mwandishi alikusudia nini aliposema, 'umoja ni nguvu?' (alama 2)
Answer
Kwamba wote shuleni wakishirikiana – wavulana kwa wasichana – watafanikiwa kuliko kila mmoja peke yake.
Wanafunzi wa shule zinazofanya vizuri.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Ni tatizo gani walilokuwa wakikumbana nalo wanafunzi wa shule ya Namundera? (alama 2)Question 8
- Andika methali moja iliyotajwa kwenye ufahamu. (alama 2)Question 9
- Kwa nini mkulima huyu anajiita mpumbavu wa kilimo? (alm 1)Question 10
- Kwa maneno yasiyozidi arobaini; andika matukio ya kisa hiki kwa ufupi? (alm 4)Question 11
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo 12.Question 12
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo 13.Question 13