CBC Grade 7 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 11
Kwa maneno yasiyozidi arobaini; andika matukio ya kisa hiki kwa ufupi? (alm 4)
From Kiswahili — End Term One Assessment 2025 (Set 6) · 4 marks · Topic: Kuandika, Ufupisho
Soma hadithi hii kisha ujibu maswali yatakayofuata.
Alikuwepo mkulima mmoja mpumbavu ambaye hakutambua madhara ya upumbavu wake. Alipata matokeo duni kinyume na malengo aliyojiwekea. Mkulima huyu alitafuta shamba kubwa na kujinasibu kuwa msimu wa wakati huo hakuna ambaye angeweza kuvuna kumshinda hata wale wataalamu wa kilimo cha kisasa wanaotumia matrekta na mitambo ya kisasa. Ilipofika wakati wa kuandaa shamba, wafanyikazi wake waliandaa vyema wakimsubiri bosi wao awaelekeze jambo la kufanya. Baadaye waliamua kupanda mbegu kwa ustadi mkubwa na kwa malengo ya kupata mavuno mengi kutokana na usasa wa mbegu na viwango vya upanzi walivyotumia.
Mkulima yule alipofika shambani, aliwaamuru watumishi wale wasafishe kila uchafu shambani na waukusanye kwa kuwa uchafu ule ulikuwa na thamani sana. Basi walikusanya na ikafika wakati wakakusanya mpaka mbegu walizopanda. Mkulima yule akawasihi wafukue kila mahali na punje na nafaka zote zirudishwe ghalani. Kazi ilifanywa vyema na wapagazi wale. Kwa kuwa pia walimuogopa mkulima yule walihakikisha hakuna punje ya nafaka iliyosalia ardhini. Kwa majigambo makubwa mkulima aliamua kujinasibu kwa kuonyesha watu ni jinsi gani alivyoweza kuvuna matunda ya ukulima kabla hata ya wakati wa mavuno kufika. Aliweza pia kubeza wakulima wenzake kwamba wajiandae kisaikolojia kwani alitarajia kuvuna mara kumi ya matazamio na iwapo watapata njaa basi wasisite kuomba kwake.
Wakati wa mavuno ulipofika watu walijongea mashambani kuvuna. Mkulima mpumbavu alipigwa na butwaa kuona hakuna hata chembe ya mmea iliyoota shambani kwake. Hii ilimfanya mkulima huyo aanze kugombana na wafanyakazi, majirani na hata washauri wake wa kilimo. Bwana mmoja alimwambia mkulima waongozane mpaka ghalani alipohifadhi mavuno ya awali wakati wa kusafisha shamba. Hapo mkulima alistaajabu alipogundua kuwa nafaka zote zilizokuwa ghalani ni mbegu ambazo alipaswa kuziacha shambani zipate kumea ili aweze kuvuna. Mkulima yule ahapo ndipo alipokiri kwamba hakuwa na ujuzi kuhusu kilimo na hata walipomshauri hakutaka kusikia hivyo yeye ni MPUMBAVU wa kilimo.
11. Kwa maneno yasiyozidi arobaini; andika matukio ya kisa hiki kwa ufupi? (alm 4)
Answer
Mkulima mpumbavu alijigamba angevuna sana. Wafanyakazi walipanda mbegu vizuri, lakini aliwaamuru wasafishe shamba na kukusanya hata mbegu. Wakati wa mavuno hakuna kilichoota. Aligundua mbegu zilikuwa ghalani, akakiri hana ujuzi wa kilimo.
Matukio makuu tu.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo 12.Question 12
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo 13.Question 13
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo 14.Question 14
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo 15.Question 15
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo 16.Question 16
- SEHEMU YA C: SARUFI Andika wingi wa nomino hizi. 17. upishiQuestion 17