naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 34

(d) Andika methali moja inayoambatana na hadithi hii? (alama 2)

From Kiswahili — End Term One Assessment 2025 (Set 6) · 2 marks · Topic: Fasihi, Methali

Soma hadithi hii kisha ujibu maswali yatakayofuata.
Mara nyingi adhabu na nidhamu huwachanganya watu. Wao huweka mipaka madhubuti ambayo ikikiukwa matokeo ni adhabu kali. Adhabu aghalabu hutolewa kama malipo kwa kosa lililotendeka. Je, kuna njia nyingine?
Dini hupendekeza kwamba kumuasa mwerevu ni bora kuliko kumchapa mjinga mara mia moja. Wataalamu wengi wanaashiria kuwa ikiwa ni lazima, basi kiboko kitumike tu iwapo njia nyingine zote zimeambulia patupu. Wanaamini kwamba kuchapa mara kwa mara hakubadili mienendo mibaya bali uendeleza dhana ya kwamba kosa ni kosa ikiwa litagunduliwa na adhabu kutolewa. Umuhimu wa nidhamu bila ya kukadiria adhabu iambatanayo ni uvunjaji wa sheria.
Kufunza nidhamu kunafaa zaidi kabla ya tendo kufanyika. Ni muhimu, kwa mfano katika shule zetu, wanafunzi kuelezwa yanayokubalika na yasiyokubalika katika mazingira yao; kutilia mkazo umuhimu wa kutii na kutenda wema kuliko kutoa adhabu mtu anapokosa. Mambo mengine yaweza kufunzwa kwa kusisitiza manufaa ya kuwa na nidhamu bora. Kwa mfano, mwanafunzi akitenda wema, asifiwe na kuhimizwa kushikilia mkondo huo. Hili litendwe hadharani. Kwa upande mwingine, ukosefu wa nidhamu usipewe nafasi ya kunawiri bali ukomeshwe haraka iwezekanavyo. Wanafunzi, kupitia ushauri wa mara kwa mara, wahimizwe kujieleza kupitia kwa maneno badala ya hisia zao kudhihiri kupitia kwa matendo maovu. wahusishwe katika kuamua mambo yanayowahusu.

(d) Andika methali moja inayoambatana na hadithi hii? (alama 2)

Answer

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test