CBC Grade 7 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 33
(c) Kulingana na hadithi, taja njia mbili za adhabu (alama 2)
From Kiswahili — End Term One Assessment 2025 (Set 6) · 2 marks · Topic: Fasihi, Hadithi
Soma hadithi hii kisha ujibu maswali yatakayofuata.
Mara nyingi adhabu na nidhamu huwachanganya watu. Wao huweka mipaka madhubuti ambayo ikikiukwa matokeo ni adhabu kali. Adhabu aghalabu hutolewa kama malipo kwa kosa lililotendeka. Je, kuna njia nyingine?
Dini hupendekeza kwamba kumuasa mwerevu ni bora kuliko kumchapa mjinga mara mia moja. Wataalamu wengi wanaashiria kuwa ikiwa ni lazima, basi kiboko kitumike tu iwapo njia nyingine zote zimeambulia patupu. Wanaamini kwamba kuchapa mara kwa mara hakubadili mienendo mibaya bali uendeleza dhana ya kwamba kosa ni kosa ikiwa litagunduliwa na adhabu kutolewa. Umuhimu wa nidhamu bila ya kukadiria adhabu iambatanayo ni uvunjaji wa sheria.
Kufunza nidhamu kunafaa zaidi kabla ya tendo kufanyika. Ni muhimu, kwa mfano katika shule zetu, wanafunzi kuelezwa yanayokubalika na yasiyokubalika katika mazingira yao; kutilia mkazo umuhimu wa kutii na kutenda wema kuliko kutoa adhabu mtu anapokosa. Mambo mengine yaweza kufunzwa kwa kusisitiza manufaa ya kuwa na nidhamu bora. Kwa mfano, mwanafunzi akitenda wema, asifiwe na kuhimizwa kushikilia mkondo huo. Hili litendwe hadharani. Kwa upande mwingine, ukosefu wa nidhamu usipewe nafasi ya kunawiri bali ukomeshwe haraka iwezekanavyo. Wanafunzi, kupitia ushauri wa mara kwa mara, wahimizwe kujieleza kupitia kwa maneno badala ya hisia zao kudhihiri kupitia kwa matendo maovu. wahusishwe katika kuamua mambo yanayowahusu.
(c) Kulingana na hadithi, taja njia mbili za adhabu (alama 2)
Answer
Kuchapa kwa kiboko na kuasa (kuonya).
Kiboko na maonyo.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- (d) Andika methali moja inayoambatana na hadithi hii? (alama 2)Question 34
- Makala haya yanazungumzia juu ya nini? (alama 1)Question 1
- Taja umuhimu wa miti kwa watu. (alama 2)Question 2
- Ni kipi kilichofanyika duniani baada ya kutambua umuhimu wa miti? (alama 2)Question 3
- Andika msemo uliotajwa kuhusiana na ukataji wa miti. (alama 1)Question 4
- Hotuba hii ilikuwa ikitolewa na nani? (alama 1)Question 5