naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2026 · Question 8

(d) Taja mbinu za lugha zilizotumiwa katika vifungu vifuatavyo. (Alama 3) (i) Amechana mbuga (ii) Aulize maswali mfululizo kama cherehani (iii) Alilivalia njuga

From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 3 marks · Topic: Kusoma, Novela

Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali.

Bahati alisahau kuhusu maisha yake machungu. Aliwasahau ndugu zake na mamake wa kambo. Ni mara moja tu alijikuta akijiuliza watu hao walifanya nini walipogundua kuwa amechana mbuga. Pia, alitamani kujua wangefanya nini ikiwa wangeona maisha aliyokuwa akiishi. Kila mawazo hayo yalipomjia, Bahati aliyasukuma nje ya akili yake. Haikuwa na maana yoyote kuwaweka watu waliomdhulumu akilini na moyoni.

Siku zilienda mbio nyumbani kwa Bwana Patel. Kwa sababu ya lishe bora na kutunzwa vizuri, Bahati alikua haraka. Akili zake zilizidi kushika mambo kwa wepesi wa ajabu. Aliifufua ndoto yake ya kuwa daktari. Darasani na nyumbani aliuliza maswali bila kikomo. Hamu yake ya kutaka kujua mambo ilimfanya aulize maswali mfululizo kama cherehani. Siku moja, baada ya kiamshakinywa, Bahati alimuuliza Bwana Patel swali gumu.

“Mbona kampuni ya ujenzi ya Shang ilimwua babangu?” Patel alitokwa na jasho akashindwa amwambie nini Bahati. Alikuwa ameisikia kampuni hiyo lakini hakuwa na habari kuwa Mokua alifanya kazi huko.

Patel alilivalia njuga suala la kifo cha Mokua ili apate kumridhisha Bahati. Alizungukazunguka kuwahoji wafanyakazi wa kampuni hiyo kuhusu kifo cha Mokua. Mfanyakazi mmoja alimweleza kila kitu dhahiri shahiri. Alimweleza kuwa Mokua alifariki kutokana na ajali iliyotokea huko kazini. Baada ya kifo chake wafanyakazi wachache walijaribu kufuatilia suala la fidia lakini juhudi zao zikaambulia patupu.

(d) Taja mbinu za lugha zilizotumiwa katika vifungu vifuatavyo. (Alama 3)
(i) Amechana mbuga
(ii) Aulize maswali mfululizo kama cherehani
(iii) Alilivalia njuga

Answer

(i) Nahau (ii) Tashbihi (iii) Nahau

"Kuchana mbuga" (kutoroka) na "kuvalia njuga" (kushughulikia jambo kwa bidii) ni nahau. "Kama cherehani" ni tashbihi kwa kuwa inalinganisha kwa "kama".

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test