CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2026 · Question 5
ZOEZI III: NOVELA (alama 10) (a) Taja wahusika wawili katika sehemu hii ya novela. (Alama 2)
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 2 marks · Topic: Kusoma, Novela
Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali.
Bahati alisahau kuhusu maisha yake machungu. Aliwasahau ndugu zake na mamake wa kambo. Ni mara moja tu alijikuta akijiuliza watu hao walifanya nini walipogundua kuwa amechana mbuga. Pia, alitamani kujua wangefanya nini ikiwa wangeona maisha aliyokuwa akiishi. Kila mawazo hayo yalipomjia, Bahati aliyasukuma nje ya akili yake. Haikuwa na maana yoyote kuwaweka watu waliomdhulumu akilini na moyoni.
Siku zilienda mbio nyumbani kwa Bwana Patel. Kwa sababu ya lishe bora na kutunzwa vizuri, Bahati alikua haraka. Akili zake zilizidi kushika mambo kwa wepesi wa ajabu. Aliifufua ndoto yake ya kuwa daktari. Darasani na nyumbani aliuliza maswali bila kikomo. Hamu yake ya kutaka kujua mambo ilimfanya aulize maswali mfululizo kama cherehani. Siku moja, baada ya kiamshakinywa, Bahati alimuuliza Bwana Patel swali gumu.
“Mbona kampuni ya ujenzi ya Shang ilimwua babangu?” Patel alitokwa na jasho akashindwa amwambie nini Bahati. Alikuwa ameisikia kampuni hiyo lakini hakuwa na habari kuwa Mokua alifanya kazi huko.
Patel alilivalia njuga suala la kifo cha Mokua ili apate kumridhisha Bahati. Alizungukazunguka kuwahoji wafanyakazi wa kampuni hiyo kuhusu kifo cha Mokua. Mfanyakazi mmoja alimweleza kila kitu dhahiri shahiri. Alimweleza kuwa Mokua alifariki kutokana na ajali iliyotokea huko kazini. Baada ya kifo chake wafanyakazi wachache walijaribu kufuatilia suala la fidia lakini juhudi zao zikaambulia patupu.
ZOEZI III: NOVELA (alama 10)
(a) Taja wahusika wawili katika sehemu hii ya novela. (Alama 2)
Answer
Bahati na Bwana Patel.
Wahusika wanaotajwa ni Bahati, Bwana Patel, Mokua (babake Bahati) na mfanyakazi wa kampuni ya Shang.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- (b) Taja mandhari yanayojitokeza katika sehemu hii ya novela. (Alama 1)Question 6
- (c) Jadili aina mbili za maudhui yaliyoangaziwa katika sehemu hii ya novela. (Alama 4)Question 7
- (d) Taja mbinu za lugha zilizotumiwa katika vifungu vifuatavyo. (Alama 3) (i) Amechana mbuga (ii) Aulize maswali…Question 8
- ZOEZI IV: WIMBO (ALAMA 10) (a) Nyimbo za aina hii huitwaje? (Alama 1)Question 9
- (b) Eleza mazingira ambamo nyimbo za aina hii huimbwa. (Alama 2)Question 10
- (c) Jadili sifa zozote tatu za nyimbo za aina hii zinazojitokeza katika wimbo huu. (Alama 3)Question 11