CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 15
Ni lipi kati ya yafuatayo ni chanzo cha ukosefu wa usalama?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 4) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu swali la 14 hadi 20.
Ukosefu wa usalama ni hali ambapo watu hawako huru kuishi bila hofu ya kudhuriwa au kupoteza mali zao. Hali hii inaweza kusababishwa na mambo kama uhalifu, vita, ukosefu wa ajira, matumizi ya dawa za kulevya, au ukosefu wa usalama, watu huishi kwa wasiwasi na mara nyingi hushindwa kufanya shughuli zao za kila siku kwa ufanisi, kama vile biashara au masomo.
Madhara ya ukosefu wa usalama ni makubwa kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Kwanza, husababisha vifo, majeraha na uharibifu wa mali, vilevile hupunguza maendeleo ya kiuchumi kwa sababu wawekezaji hukwepa maeneo yasiyo salama. Pia watoto wanaweza kushindwa kwenda shule na hivyo kuathiri elimu yao. Aidha, ukosefu wa usalama husababisha hofu na msongo wa mawazo miongoni mwa wananchi, jambo linalodhoofisha mshikamano wa kijamii.
15. Ni lipi kati ya yafuatayo ni chanzo cha ukosefu wa usalama?
- AElimu bora
- BUhalifu
- CMichezo
- DUsafi wa mazingira
Answer
B. Uhalifu
Uhalifu husababisha ukosefu wa usalama.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Watu katika jamii yenye ukosefu wa usalama huishi vipi?Question 16
- Ukosefu wa usalama unaathiri vipi biashara?Question 17
- Neno ajira limetumika katika kifungu hiki, ni sawa kimaana na?Question 18
- Ukosefu wa usalama huathiri vipi elimu ya watoto?Question 19
- Wawekezaji hufanya nini katika maeneo yasiyo salama?Question 20
- Je, mazungumzo haya yanafanyika wakati gani?Question 21