naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 13

Ni nini maana ya “tukakubali kwa kuwa hatukuwa na budi?

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 3) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu swali la 8 hadi 13.
Wageni tuliowaalika kutoka Ugiriki walituwekea masharti magumu. Walikataa katakata kuchukuliwa hotelini au kuletewa chakula cha hoteli. Tukakubali kwa kuwa hatukuwa na budi.
Walipofika tu, walijigawa, wengine wakabaki sebuleni na wengine wakaenda moja kwa moja hadi jikoni. Do! Kumbe kilichowaleta mapema mno ni kutaka kuona mapishi yetu.
Kwa hakika walituwahi vizuri. Mimi binafsi nilikuwa na kinu na mchi nikitwanga maharagwe. Shangazi alikuwa juu ya mbuzi akikuna nazi huku malkia akimsaidia kuichuja nazi hiyo kwa kifumbu ili apate tui na machicha. Halati akawa yuampara samaki huku Amati akiunga mchuzi kwa viungo alivyokuwa amevitayarisha. Nyanya alikuwa akidondoa mchele kuondoa ndume ilhali wifi zangu walikuwa wakiambua viazi, kuoka mikate na kukoka moto. Jirani yetu Bidii alikuwa akikanda unga na baadaye kuisukuma mikate.

13. Ni nini maana ya “tukakubali kwa kuwa hatukuwa na budi?

  1. AKwa kuwa tulikuwa hatuna kazi nyingine.
  2. BKwa furaha ya kupunguza gharama.
  3. CTulikubali kwa sababu ilitulazimu.
  4. DTulikubali shingo upande.

Answer

C. Tulikubali kwa sababu ilitulazimu.

Kutokuwa na budi ni kulazimika.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test