naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 17

d) Taja na ueleze mbinu za lugha ambazo zimetumika katika riwaya hii. (Alama 3)

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 2) · 3 marks · Topic: Kusoma, Riwaya

ZOEZI LA 4: RIWAYA - Mshale wa matumaini
Soma kifungu hiki, kisha uyajibu maswali.
Niliwaza kuhusu safari iliyobakia. Miguu tayari ilikuwa ikiniuma nyayoni na magotini, pia nilihisi maumivu fulani ya kifuani nyongoni, sikutaka mama yangu ajue nilikuwa na maumivu, sikutaka kumwongezea mama yangu adha zaidi, alikuwa na matatizo yakutosha.
Nilichukua kitabu changu cha Mshale wa Matumaini ili kujiliwaza. Nilifungua ukursa niliokuwa nimeachia awali na kuendelea.
“Hakuna mwanadamu aliyeumbwa na akili isiyofikiria, labda awe na hitilafu ya ubongo. Kama unaweza kuwaza na kuamua basi unaweza kutumia akili yako na kujiinua na kujiendeleza. Mtu yeyote yule afanye mambo ya kihayawani kama vile ukatili na kumwaga damu unyang’anyi, uporaji na unyanyasaji wa wanyonge; mtu huyo hata tofauti na hayawani kwani hatumii akili yake vyema ili kuboresha maisha yake na ya watu wanaomzunguka......”
Wakati nilipokuwa nikisoma, wakimbizi wengi walionekana wakiwa wamechoka tiki. Kuna wale waliolala fofofo. Wengine wachache waliozungumza kwa sauti za chinichini lakini ungeweza kukadiria uchovu waliokua nao. Maisha yaliokuwa ya tabu. Lakini mtu aling’ang’ana kuishi. Hapana aliyetamani kuachwa nyuma.
Chakula hatimaye kiliiva. Tulipakuliwa katika sahani za plastiki zilizotoka ofisi ya chifu. Ilikuwa vigumu kuonana vizuri kwasababu ya mishumaa iliyotumika.
Nilikuwa nishazoea taa za umeme kwetu nyumbani. Siku hio ilinibidi kutumia mwanga wa mshuma. Ilikuwa vigumu kwangu kutumia.

d) Taja na ueleze mbinu za lugha ambazo zimetumika katika riwaya hii. (Alama 3)

Answer

Tanakali ya sauti: "kuchoka tiki", "walilala fofofo"; utohozi: "plastiki"; nafsi ya kwanza katika usimulizi.

Tafuta maneno yanayoigiza hali na maneno ya kigeni.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test