CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 5
Maswali a) Shairi hili huitwa tarbia. Kwa nini? (Alama 2)
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 2) · 2 marks · Topic: Kusoma, Ushairi
ZOEZI LA 3: SHAIRI (Alama 10)
Soma shairi hili kisha uyajibu maswali yafuatayo.
Kijana nenda usome, masomo yako shuleni
Kuchezacheza ukome, siri imo vitabuni
Kwa imara usimame, uvivu ni kitu duni
Kijana nenda usome, elimu ndiyo maisha
Maisha leo magumu, usiposoma hatari,
Hupati vitu muhimu, nguo mlo na sukari,
Kwanza uwe na elimu, ndipo uwe mashuhuri
Kijana nenda usome, elimu ndiyo maisha.
Mahitaji sasa mengi, bila pesa huyapati
Maisha ala msingi, hulivai hata shati
Soma uwe serehongi, mtalamu mtafiti
Kijana nenda usome, elimu ndiyo maisha
Maisha kama sunami, ni tufani yenye nguvu
Bila akili kichwani, utaitwa mpumbavu
Usome sana shuleni, usikubali uvivu
Kijana nenda usome, elimu ndiyo maisha
Beti tano nimefika, elimu ina faida,
Ndiyo mali ya kuweka, inayoleta msaada,
Mtu akielimika, ajipunguzia shida
Kijana nenda usome, elimu ndiyo maisha
Maswali
a) Shairi hili huitwa tarbia. Kwa nini? (Alama 2)
Answer
Kwa sababu kila ubeti una mishororo minne.
Hesabu mistari ya kila ubeti.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- b) Shairi hili lina beti ngapi? (Alama 2)Question 6
- c) Kipokokeo cha shairi hili ni gani? (Alama 2)Question 7
- d) Ukitolea, mifano andika mbinu za lugha ambazo zimetumika katika shairi hili. (Alama 2)Question 8
- e) Andika vina vya kati na vya mwisho vya ubeti wa tano. (Alama 2)Question 9
- Maswali a) Eleza sifa za tamthilia zinazojitokeza katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 2)Question 10
- b) Ukitoa mifano, andika mbinu za lugha ambazo zimetumika kwenye kifungu hiki. (Alama 4)Question 11