CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 9
e) Andika vina vya kati na vya mwisho vya ubeti wa tano. (Alama 2)
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 2) · 2 marks · Topic: Kusoma, Ushairi
ZOEZI LA 3: SHAIRI (Alama 10)
Soma shairi hili kisha uyajibu maswali yafuatayo.
Kijana nenda usome, masomo yako shuleni
Kuchezacheza ukome, siri imo vitabuni
Kwa imara usimame, uvivu ni kitu duni
Kijana nenda usome, elimu ndiyo maisha
Maisha leo magumu, usiposoma hatari,
Hupati vitu muhimu, nguo mlo na sukari,
Kwanza uwe na elimu, ndipo uwe mashuhuri
Kijana nenda usome, elimu ndiyo maisha.
Mahitaji sasa mengi, bila pesa huyapati
Maisha ala msingi, hulivai hata shati
Soma uwe serehongi, mtalamu mtafiti
Kijana nenda usome, elimu ndiyo maisha
Maisha kama sunami, ni tufani yenye nguvu
Bila akili kichwani, utaitwa mpumbavu
Usome sana shuleni, usikubali uvivu
Kijana nenda usome, elimu ndiyo maisha
Beti tano nimefika, elimu ina faida,
Ndiyo mali ya kuweka, inayoleta msaada,
Mtu akielimika, ajipunguzia shida
Kijana nenda usome, elimu ndiyo maisha
e) Andika vina vya kati na vya mwisho vya ubeti wa tano. (Alama 2)
Answer
Vina vya kati: -ka, -ka, -ka, -me. Vina vya mwisho: -da, -da, -da, -sha.
Angalia silabi za mwisho katika kila kipande cha mstari.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Maswali a) Eleza sifa za tamthilia zinazojitokeza katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 2)Question 10
- b) Ukitoa mifano, andika mbinu za lugha ambazo zimetumika kwenye kifungu hiki. (Alama 4)Question 11
- c) Eleza sifa za Mishi kulingana na kifungu hiki. (Alama 2)Question 12
- d) Fafanua mandhari ambayo yametumika katika kifungu hiki. (Alama 2)Question 13
- Maswali a) Eleza maudhui ambayo yameangaziwa katika kifungu hiki. (Alama 4)Question 14
- b) Dhamira ya mwandishi katika kifungu hiki ni (Alama 2)Question 15