naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 11

b) Ukitoa mifano, andika mbinu za lugha ambazo zimetumika kwenye kifungu hiki. (Alama 4)

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 2) · 4 marks · Topic: Kusoma, Tamthilia

ZOEZI LA 4: TAMTHILIA - Wema hauozi - Onyesho III
(Mahali palepale. Usiku wa maneno. Mishi bado ameketi alipokuwa katika Onyesho II japo sasa anasinziasinzia. Sweta anayofuma inamponyokaponyoka. Mara yanasikika matiti ya mtu anayetembea. Kisha anaonyesha wasiwasi. Mara mlango unabishwa)
Mishi: Ni nani? (Mlango unabishwa tena. Mara hii anajibu kwa woga) Ninauliza ni nani? (Hakuna jibu badala yake unabishwa tena. Anaonyesha woga mkumbwa.) Kama husemi nitapiga kamaso. Watu wakitoka watakuadhibu. (Kinasikika kicheko kirefu kutoka nje)
Mabula: Fungua!
Mishi: (Anatulia japo amekasirika. Anakwenda kufungua mlango). Haki Mabula! Mbona hivyo?
Mabula: (Anaingia huku anaonyesha dalili za kulewa) Kwani kuna nini?
Mishi: Umenitisha karibu roho initoke!
Mabula: Si wewe uliniambia kuwa siwezi kukutisha? Sasa ona, jambo dogo limekutoa kamasi jembamba.
Mishi: Umenistua sana!
Mabula: Sasa umeona kuwa bado ninaweza kukushitua. Nilitaka tu ufahamu hivyo (huku anaketi). Otherwise kikao cha wazee kimekwenda vizuri.
Mishi: Kila ukikuja usiku kama hivi unakuja na habari za ‘kikao cha wazee’. Wanasema panapo wazee hapaharibiki neno lakini hivi vikao vyenu havina hujambo yoyote siku hadi siku! Muda unapotezwa bure tu!
Mabula: Mishi ona sasa. Mimi hata sijafika nikatulia. Malalamishi kutoka kwako moja kwa moja. Kumbuka ndio yalionifukuza nyumbani alasiri. Nimeenda kwa wazee wenzangu kujipumbaza walau kuona kama usiku itapita bila kubwa lakini wapi! Umeniandama kama kivuli.

b) Ukitoa mifano, andika mbinu za lugha ambazo zimetumika kwenye kifungu hiki. (Alama 4)

Answer

Nidaa: "Fungua!"; tashhisi: "roho itoke"; tashbihi: "umeniandama kama kivuli"; utohozi: "sweta".

Tafuta alama za hisi, ulinganisho na maneno ya kigeni.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test