CBC Grade 7 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 12
c) Eleza sifa za Mishi kulingana na kifungu hiki. (Alama 2)
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 2) · 2 marks · Topic: Kusoma, Tamthilia
ZOEZI LA 4: TAMTHILIA - Wema hauozi - Onyesho III
(Mahali palepale. Usiku wa maneno. Mishi bado ameketi alipokuwa katika Onyesho II japo sasa anasinziasinzia. Sweta anayofuma inamponyokaponyoka. Mara yanasikika matiti ya mtu anayetembea. Kisha anaonyesha wasiwasi. Mara mlango unabishwa)
Mishi: Ni nani? (Mlango unabishwa tena. Mara hii anajibu kwa woga) Ninauliza ni nani? (Hakuna jibu badala yake unabishwa tena. Anaonyesha woga mkumbwa.) Kama husemi nitapiga kamaso. Watu wakitoka watakuadhibu. (Kinasikika kicheko kirefu kutoka nje)
Mabula: Fungua!
Mishi: (Anatulia japo amekasirika. Anakwenda kufungua mlango). Haki Mabula! Mbona hivyo?
Mabula: (Anaingia huku anaonyesha dalili za kulewa) Kwani kuna nini?
Mishi: Umenitisha karibu roho initoke!
Mabula: Si wewe uliniambia kuwa siwezi kukutisha? Sasa ona, jambo dogo limekutoa kamasi jembamba.
Mishi: Umenistua sana!
Mabula: Sasa umeona kuwa bado ninaweza kukushitua. Nilitaka tu ufahamu hivyo (huku anaketi). Otherwise kikao cha wazee kimekwenda vizuri.
Mishi: Kila ukikuja usiku kama hivi unakuja na habari za ‘kikao cha wazee’. Wanasema panapo wazee hapaharibiki neno lakini hivi vikao vyenu havina hujambo yoyote siku hadi siku! Muda unapotezwa bure tu!
Mabula: Mishi ona sasa. Mimi hata sijafika nikatulia. Malalamishi kutoka kwako moja kwa moja. Kumbuka ndio yalionifukuza nyumbani alasiri. Nimeenda kwa wazee wenzangu kujipumbaza walau kuona kama usiku itapita bila kubwa lakini wapi! Umeniandama kama kivuli.
c) Eleza sifa za Mishi kulingana na kifungu hiki. (Alama 2)
Answer
Ni mwenye malalamishi (analalamika kuhusu vikao vya wazee) na mwoga (anaogopa mlango unapobishwa); pia ni mwenye hasira.
Angalia anavyojibu mlango unapobishwa na anavyomwambia Mabula.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- d) Fafanua mandhari ambayo yametumika katika kifungu hiki. (Alama 2)Question 13
- Maswali a) Eleza maudhui ambayo yameangaziwa katika kifungu hiki. (Alama 4)Question 14
- b) Dhamira ya mwandishi katika kifungu hiki ni (Alama 2)Question 15
- c) “Kuchoka tiki” ni mbinu gani ya lugha. (Alama 1)Question 16
- d) Taja na ueleze mbinu za lugha ambazo zimetumika katika riwaya hii. (Alama 3)Question 17
- ZOEZI LA 1: INSHA (Alama 15) Andika insha juu ya: UMOJA NI NGUVU, UTENGANO NI UDHAIFU.Question 1