CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 9
Kulingana na aya ya mwisho ni kweli kusema kuwa
From Test 21 — Grade 6 Revision Paper 1, 2026 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Kifungu cha Ufahamu
Kasomi alikuwa mwanafunzi wa darasa la sita. Hakuwa mwerevu sana na pia hakuwa samaki. Kwa kweli, hakuna mwanafunzi mjinga sana ambaye hawezi kufunzwa akaelewa. Ukimwona mtoto anashindwa kuelewa masomo darasani, yeye mwenyewe ameamua kwamba hataki kusoma wala kuelewa. Na ukiona ameamua hivyo, yeye ana mambo mengine kichwani na moyoni ambayo anayashughulikia yakachukua nafasi ya masomo. Kumbuka, huwezi kutumikia vitu viwili kwa wakati mmoja.
Huwezi kupanda farasi wawili kwa wakati mmoja. Njia mbili zilimshinda hata fisi na ulafi wake.
Kasomi alianza kuwa duni darasani. Jambo hili lilinishangaza. Mbona kitambo alikuwa chapuchapu? Mbona kitambo alikuwa akijifunga nira?
Aliuliza maswali na kuyajibu mengine darasani. Maswali haya yalinisumbua mpaka siku moja nikaanza kuchunguza mienendo yake. Nikagundua kuwa yeye hurudi darasani kisirisiri wakati wengine wako uwanjani wakicheza. Humo alipekuapekua mikoba na madawati ya wenzake akachukua vya kuchukua. Alikuwa mwizi! Leo amekamatwa. Aibu! Wizi na masomo, ni kipi bora?

- AKasomi alikuwa mwaminifu
- BKasomi alikuwa mtundu
- CKasomi alikuwa mlokole
- DKasomi alikuwa na aibu
Answer
B. Kasomi alikuwa mtundu
Aya ya mwisho inaonyesha Kasomi akiwaibia wenzake mikoba na madawati kisirisiri -- tabia ya utundu na uzandiki.
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Ni mwanafunzi yupi alitaja chombo ambacho huendeshwa majini?Question 10
- Chagua chombo ambacho hubeba abilia wachache kabisa.Question 11
- Ni chombo kipi huwa na rubani?Question 12
- Ni kweli kusema kuwaQuestion 13
- Serikali za nchi zinahimizwa kufanya nini?Question 14
- Ni jukumu la nani kudumisha usafi wa mazingira?Question 15