naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 15

Ni jukumu la nani kudumisha usafi wa mazingira?

From Test 21 — Grade 6 Revision Paper 1, 2026 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu

Kifungu cha Ufahamu
Ugonjwa wa malaria ni tishio kubwa kwa afya na uhai wa watoto walio chini ya miaka mitano. Ugonjwa huu umeenea hasa maeneo ya Ziwa Victoria. Kulingana na ripoti ya shirika la Afya Duniani, WHO, malaria huambukizwa na mbu wa kike kwa jina Anofelesi.
Mbu husambaza malaria kwa kufyonza damu za watu mbalimbali. Ripoti inasema kuwa, watoto zaidi ya elfu mbili huaga dunia humu nchini kutokana na makali ya malaria. Umoja wa mataifa unahimiza nchi kuweka mikakati kabambe kukabaliana na tatizo la malaria. Serikali kuu ikishirikiana na serikali za kaunti imejifunga kibwebwe na kuweka mikakati ya kupambana na jinamizi hili.
Neti zilizopakwa dawa zimesambazwa kote nchini. Kila mwananchi anahitajika kupokea neti hizo bila malipo. Neti hizo zina dawa ya kuua mbu. Kila mwananchi anahitajika kudumisha usafi anapoishi. Akate nyasi ndefu, atoe maji yaliyotuama na kurusha mbali mikebe iliyo na maji kwani vitu hivi huwezesha mbu kutaga mayai.

Ni jukumu la nani kudumisha usafi wa mazingira?

  1. AKila mmoja
  2. BSerikali nchini
  3. CShirika la afya
  4. DUmoja wa mataifa

Answer

A. Kila mmoja

Kifungu kinasema "Kila mwananchi anahitajika kudumisha usafi anapoishi", likimaanisha ni jukumu la kila mmoja.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test