naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 8

Ni nini maana ya nahau akijifunga nira?

From Test 21 — Grade 6 Revision Paper 1, 2026 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Nahau na Semi

Kifungu cha Ufahamu
Kasomi alikuwa mwanafunzi wa darasa la sita. Hakuwa mwerevu sana na pia hakuwa samaki. Kwa kweli, hakuna mwanafunzi mjinga sana ambaye hawezi kufunzwa akaelewa. Ukimwona mtoto anashindwa kuelewa masomo darasani, yeye mwenyewe ameamua kwamba hataki kusoma wala kuelewa. Na ukiona ameamua hivyo, yeye ana mambo mengine kichwani na moyoni ambayo anayashughulikia yakachukua nafasi ya masomo. Kumbuka, huwezi kutumikia vitu viwili kwa wakati mmoja.
Huwezi kupanda farasi wawili kwa wakati mmoja. Njia mbili zilimshinda hata fisi na ulafi wake.
Kasomi alianza kuwa duni darasani. Jambo hili lilinishangaza. Mbona kitambo alikuwa chapuchapu? Mbona kitambo alikuwa akijifunga nira?
Aliuliza maswali na kuyajibu mengine darasani. Maswali haya yalinisumbua mpaka siku moja nikaanza kuchunguza mienendo yake. Nikagundua kuwa yeye hurudi darasani kisirisiri wakati wengine wako uwanjani wakicheza. Humo alipekuapekua mikoba na madawati ya wenzake akachukua vya kuchukua. Alikuwa mwizi! Leo amekamatwa. Aibu! Wizi na masomo, ni kipi bora?

Ni nini maana ya nahau akijifunga nira?

  1. AKuwa na bidii
  2. BKuwa na mabadiliko
  3. CKuwa mtundu
  4. DKuwa mtu mzuri

Answer

A. Kuwa na bidii

Nahau "kujifunga nira" humaanisha kujituma na kuwa na bidii katika jambo fulani, kama alivyokuwa Kasomi kabla ya kuwa mzembe.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test