CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 7
Mwanafunzi hukosa kuelewa masomo ikiwa
From Test 21 — Grade 6 Revision Paper 1, 2026 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Kifungu cha Ufahamu
Kasomi alikuwa mwanafunzi wa darasa la sita. Hakuwa mwerevu sana na pia hakuwa samaki. Kwa kweli, hakuna mwanafunzi mjinga sana ambaye hawezi kufunzwa akaelewa. Ukimwona mtoto anashindwa kuelewa masomo darasani, yeye mwenyewe ameamua kwamba hataki kusoma wala kuelewa. Na ukiona ameamua hivyo, yeye ana mambo mengine kichwani na moyoni ambayo anayashughulikia yakachukua nafasi ya masomo. Kumbuka, huwezi kutumikia vitu viwili kwa wakati mmoja.
Huwezi kupanda farasi wawili kwa wakati mmoja. Njia mbili zilimshinda hata fisi na ulafi wake.
Kasomi alianza kuwa duni darasani. Jambo hili lilinishangaza. Mbona kitambo alikuwa chapuchapu? Mbona kitambo alikuwa akijifunga nira?
Aliuliza maswali na kuyajibu mengine darasani. Maswali haya yalinisumbua mpaka siku moja nikaanza kuchunguza mienendo yake. Nikagundua kuwa yeye hurudi darasani kisirisiri wakati wengine wako uwanjani wakicheza. Humo alipekuapekua mikoba na madawati ya wenzake akachukua vya kuchukua. Alikuwa mwizi! Leo amekamatwa. Aibu! Wizi na masomo, ni kipi bora?

- Aanawaza kuhusu masomo
- Bana mambo mengi anawaza
- Chuwa haelewi kusoma
- Dhuwa ana tabia za kuudhi
Answer
B. ana mambo mengi anawaza
Kifungu kinaeleza kuwa mwanafunzi anayeshindwa kuelewa masomo huwa ana "mambo mengine kichwani na moyoni" yanayochukua nafasi ya masomo.
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Ni nini maana ya nahau akijifunga nira?Question 8
- Kulingana na aya ya mwisho ni kweli kusema kuwaQuestion 9
- Ni mwanafunzi yupi alitaja chombo ambacho huendeshwa majini?Question 10
- Chagua chombo ambacho hubeba abilia wachache kabisa.Question 11
- Ni chombo kipi huwa na rubani?Question 12
- Ni kweli kusema kuwaQuestion 13