naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 13

Ni kweli kusema kuwa

From Test 21 — Grade 6 Revision Paper 1, 2026 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu

Kifungu cha Ufahamu
Ugonjwa wa malaria ni tishio kubwa kwa afya na uhai wa watoto walio chini ya miaka mitano. Ugonjwa huu umeenea hasa maeneo ya Ziwa Victoria. Kulingana na ripoti ya shirika la Afya Duniani, WHO, malaria huambukizwa na mbu wa kike kwa jina Anofelesi.
Mbu husambaza malaria kwa kufyonza damu za watu mbalimbali. Ripoti inasema kuwa, watoto zaidi ya elfu mbili huaga dunia humu nchini kutokana na makali ya malaria. Umoja wa mataifa unahimiza nchi kuweka mikakati kabambe kukabaliana na tatizo la malaria. Serikali kuu ikishirikiana na serikali za kaunti imejifunga kibwebwe na kuweka mikakati ya kupambana na jinamizi hili.
Neti zilizopakwa dawa zimesambazwa kote nchini. Kila mwananchi anahitajika kupokea neti hizo bila malipo. Neti hizo zina dawa ya kuua mbu. Kila mwananchi anahitajika kudumisha usafi anapoishi. Akate nyasi ndefu, atoe maji yaliyotuama na kurusha mbali mikebe iliyo na maji kwani vitu hivi huwezesha mbu kutaga mayai.

Mchoro wa mtoto mdogo akilia huku mbu kadhaa wakimzunguka na kumuuma.

Ni kweli kusema kuwa

  1. Augonjwa wa malaria hutishia maisha
  2. Bugonjwa wa malaria hauleti mauti
  3. Cugonjwa wa malaria huua wanyama
  4. Dugonjwa wa malaria si hatari

Answer

A. ugonjwa wa malaria hutishia maisha

Kifungu kinasema wazi kuwa "Ugonjwa wa malaria ni tishio kubwa kwa afya na uhai wa watoto", hivyo hutishia maisha.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test