naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 5

Chagua neno lenye maana sawa na wiki.

From Test 21 — Grade 6 Revision Paper 1, 2026 (Lugha) · 1 mark · Topic: Sarufi na Matumizi ya Lugha, Visawe

Mazungumzo
(Ni ofisini mwa Hasani ambapo Mosi anabisha)
Mosi: Hodi! hodi! Masalkheri mwenye nyumba? Mimi ni Mosi na ningetaka kujua zaidi kuhusu nyumba zako. Una nyumba ngapi na ziko wapi?
Hasan: __1__, Mosi. Nina furaha kukutana nawe ofisini mwangu hapa mjini Nairobi, Kenya. Nina nyumba nyingine katika nchi jirani.
Mosi: Vizuri sana! Ninaweza kuishi mahali popote! Sasa sina kazi lakini mimi ni mhandisi na ninaweza kupata kazi mahali popote.
Hasan: Unaweza ishi mahali popote. Mimi sikai nyumba moja kwa mara nyingi.
Mosi: Nafikiri ningependa kuishi karibu na Bahari ya Hindi. Nitaleta familia yangu baadaye na natumai pia wao wataogelea baharini kila siku.
Hasan: Pia pwani nina nyumba kadhaa.
Mosi: Mimi nina familia. Ninaweza kukodi nyumba ya ghorofa. Ina vyumba vingapi?
Hasan: Chumba kimoja kina vyumba vinne. Kina jiko, sebule, bafu na chumba cha kulala. Kingine kina vyumba vitatu: jiko, bafu na chumba cha kulala.
Mosi: Aha! Bei ya kodi ni ngapi kwa nyumba yenye sebule na nyumba bila sebule?
Hasan: Kodi kwa nyumba ya sebule ni elfu hamsini na mbili. Kodi kwa nyumba bila sebule ni sawa kwa sababu mtaa ni mzuri zaidi. Utalipa siku ya kwanza ya kila mwezi.
Mosi: Bei ni rahisi. Ninafurahi! Kitu ambacho ninahitaji tu ni barabara ya lami, fanicha na hospitali karibu. Ni kweli eti kila nyumba iko karibu na barabara ya lami na hospitali?
Hasan: Zote zina fanicha, barabara ya lami na hospitali. Hakuna huduma za takataka isipokuwa wewe unanunua huduma ya biashara tofauti.
Mosi: Sawa, sasa ninaweza kutia saini katika mapatano ya ukodishaji kwa nyumba ya ghorofa yenye sebule?
Hasan: Ndiyo, hapa yako mapatano ya ukodishaji. Utahamia lini?
Mosi: Wiki ijayo nitahamia! Asante sana, Hasan!
Hasan: Karibu.

Chagua neno lenye maana sawa na wiki.

  1. AMwaka
  2. BJuma
  3. CSiku
  4. DMwezi

Answer

B. Juma

"Wiki" na "juma" ni visawe -- maneno mawili yenye maana sawa ya kipindi cha siku saba.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test