CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 7
Soma kifungu kisha ujibu maswali 6 - 9. Sikukuu ya Madaraka husherehekewa kila mwaka nchini Kenya. Hii ni siku ambayo wakenya walipata madaraka ya kujitawala…
From Test 15 — Karatasi ya Marudio 2026 · 1 mark · Topic: Kusoma, Msamiati
Soma kifungu kisha ujibu maswali 6 - 9.
Sikukuu ya Madaraka husherehekewa kila mwaka nchini Kenya. Hii ni siku ambayo wakenya walipata madaraka ya kujitawala wenyewe baada ya kunyakua uhuru kutoka kwa wakoloni. Sikukuu hii husherehekewa tarehe mosi Juni.
Kwa kawaida, sikukuu hii hufanyika katika uwanja wa michezo na kuhudhuriwa na halaiki ya watu. Huwa kuna tamasha za muziki, ngoma za kitamaduni na gwaride la vikosi mbalimbali vya kijeshi. Wanahewa nao huonyesha ujuzi na ustadi wao wa kupaa angani kwa mitindo mbalimbali. Huwa ni sherehe ya kufana.
Sherehe za kuadhimisha sikukuu ya mwaka wa elfu mbili na ishirini, hata hivyo, zitakumbukwa daima. Hii ni kwa sababu zilikuwa tofauti kabisa na zote zilizotangulia. Tofauti moja kubwa ni kuwa zilifanyika katika ikulu ya rais na kuhudhuriwa na watu wachache sana, badala ya uga wa michezo na kuhudhuriwa na halaiki ya watu. Wageni waalikwa arobaini na sita tu, tena walitakikana wakae umbali wa mita moja, mtu mmoja kutoka kwa mwingine. Vile vile walitakikana wafunge barakoa kufunika vinywa na pua zao. Hakukuwa na tamasha zozote za muziki wala ngoma za kitamaduni.
Kabla ya sherehe kuanza zilifunguliwa kwa maombi. Mwombaji wa kwanza alikuwa wa dini ya kitamaduni kutoka Kajiado. Mwombaji wa pili alikuwa wa dini ya Kiislamu, naye mwombaji wa tatu alikuwa ni wa dini ya Kikristo. Waombaji wenyewe hawakuwa kwenye sherehe huko ikulu bali waliombea mahali pao pa ibada na maombi yao yakarekodiwa na kupeperushwa kwenye runinga na redio.
Wanajeshi wa nchi kavu, wanamaji na wanahewa walifanya gwaride wakiwa kwenye sare zao rasmi. Wanajeshi wenyewe walikuwa wachache sana. Wote walivalia glavu na barakoa nyeupe. Walipendeza na barakoa hizo; ungedhani ilikuwa sehemu ya sare rasmi. Kati ya Raisi na makamu wa rais walitazama sherehe kutoka juu kwenye roshani ya ikulu.
Kilele cha sherehe hii ilikuwa hotoba ya Rais. Rais alizungumzia umoja wa taifa. Aliwasifu viongozi waliotangulia kwa juhudi zao na maono yao ya kujenga taifa. Aliwataka wananchi kuungana ili kupigana na adui mmoja, ambaye pia ndiye aliyesababisha sherehe kufanyika namna zilizofanywa. Huyu si mwingine bali ni ugonjwa hatari wa korona.
Maneno “halaiki ya watu” yamepigiwa mstari. Yanamaanisha
- Awatu wachache
- Bwatu wengi
- Cwatu wakuu
- Dwatu mbalimbali
Answer
B. watu wengi
"Halaiki ya watu" ni msemo unaomaanisha umati mkubwa wa watu, yaani watu wengi.
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Soma kifungu kisha ujibu maswali 6 - 9. Sikukuu ya Madaraka husherehekewa kila mwaka nchini Kenya. Hii ni siku ambayo…Question 8
- Soma kifungu kisha ujibu maswali 6 - 9. Sikukuu ya Madaraka husherehekewa kila mwaka nchini Kenya. Hii ni siku ambayo…Question 9
- Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali yanayofuata. Sungura na ng'ombe walikuwa marafiki wa kufa kuzikana kwani…Question 10
- Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali yanayofuata. Sungura na ng'ombe walikuwa marafiki wa kufa kuzikana kwani…Question 11
- Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali yanayofuata. Sungura na ng'ombe walikuwa marafiki wa kufa kuzikana kwani…Question 12
- Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata. Siku moja, wanyama wote wa msitu wa Gungumalo walikusanyika…Question 13