CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 1
Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali. (Ni darasani ambapo wanafunzi wametulia kama maji mtungini. Ghafla mwalimu anaingia darasani.) Mwalimu: Hamjambo…
From Test 14 — Karatasi ya Marudio 2026 · 1 mark · Topic: Sarufi na Matumizi ya Lugha, Tashbihi
Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali.
(Ni darasani ambapo wanafunzi wametulia kama maji mtungini. Ghafla mwalimu anaingia darasani.)
Mwalimu: Hamjambo wanafunzi!
Wanafunzi: (wakisimama sawia) Hatujambo mwalimu, Shikamoo?
Mwalimu: Marahaba. Leo tunazungumzia umuhimu wa kamusi.
Njoroge: Kamusi? Hicho ni kitu gani?
Ali: Nimesikia watu wakiizungumzia lakini sijui hasa inavyotumika.
Salim: Mimi nina kamusi nyumbani. Lakini sina uhakika kama ni muhimu sana.
Mwalimu: Kamusi ni kitabu kinachoorodhesha maneno na maana yake.
Ali: Kwa nini tunahitaji kamusi ilhali tunaweza kutumia intaneti?
Mwalimu: Hebu fikirieni hivi, Je, tunayo intaneti kila wakati? Tunaweza kuitegemea kila wakati?
Njoroge: Hapana, mara nyingi intaneti inaweza kukosekana au kutokuwa na nguvu.
Ali: Wakati mwingine, Intaneti inaweza kuletea habari potovu na isiyo sahihi.
Salim: Kwa hivyo, Kamusi inaweza kutusaidia kujifunza hata kama hatuna intaneti?
Mwalimu: Ndio. Kamusi ni rasilimali imara ambayo tunaweza kutegemea daima na inatusaidia kijenga msingi mzuri wa lugha yetu.
"Wametulia kama maji mtungini" ni;
- AMethali
- BTashbihi
- CNahau
- DKitendawili
Answer
B. Tashbihi
"Wametulia kama maji mtungini" ni tashbihi -- hutumia neno "kama" kulinganisha hali mbili.
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Ni kweli kusema kuwa;Question 2
- Kamusi huonyesha nini?Question 3
- Chagua madhara ya intaneti;Question 4
- Kamusi ina manufaa gani kwa mwanafunzi?Question 5
- Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Hapo zamani, palikuwa na msichana mmoja aliyekuwa ameumbwa akaumbika.…Question 6
- Jina lingine la mvulana ni ghulamu. Je, jina lingine la msichana ni?Question 7