naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 6

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Hapo zamani, palikuwa na msichana mmoja aliyekuwa ameumbwa akaumbika. Alikuwa mrembo ajabu. Alipenda kujipamba…

From Test 14 — Karatasi ya Marudio 2026 · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Hapo zamani, palikuwa na msichana mmoja aliyekuwa ameumbwa akaumbika. Alikuwa mrembo ajabu. Alipenda kujipamba kwa mapambo ya aina nyingi. Alikuwa na pete kidoleni, herini masikioni, mkufu shingoni, kipini puani na bangili. Maghulamu wote walimtamani sana.

Hata hivyo, banati huyu alikuwa mwenye bidii masomoni. Alielewa kuwa mtaka cha mvunguni sharti ainame, hivyo hakutaka mchezo masomoni. Alifanya bidii na mwishowe akafaulu. Akasomea udaktari na sasa hivi yeye ni daktari mkuu katika hospitali ya Matokeo, Kaunti ya Kingomboni. Hakika bidii hulipa.

Ni mapambo gani ambayo hayajatajwa katika makala haya?

  1. AKipini
  2. BBangili
  3. CWanja
  4. DHerini

Answer

C. Wanja

Kifungu kinataja pete, herini, mkufu, kipini na bangili, lakini hakitaji "wanja" (wanja/kohl haikutajwa kamwe).

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test