CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 13
Ni ukweli kuwa kinyonga na wenzake
From Kiswahili — Monitoring Learners Progress 2025 (Set 9) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali 11-15.
Hapo zamani za kale, kinyonga hakuwa jinsi alivyo siku hizi. Alikuwa kama wanyama wengine. Hakuwa akibadilika rangi kila wakati. Siku moja, yeye na marafiki zake walialikwa katika sherehe iliyokuwa ikifanyika mjini. Yeye na wenzake waliingia katika gari na kufunga safari ya kuelekea mjini. Waliwasili mjini mwendo wa adhuhuri. Walipofika, walielekezwa mahali pa sherehe moja kwa moja. Sherehe ilipokaribia mwisho, wageni wote walielekezwa mahali pa kupata chakula. Hiyo ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa wageni waliotoka kijijini kuona matunda. Mengi walikuwa wakiyasikia tu kwenye redio na kuyaona magazetini. Kabla ya kuanza kula, walipewa onyo. Waliambiwa kuwa matunda hayo hayakuwa ya kawaida. Hakuna aliyeruhusiwa kula zaidi ya aina moja ya matunda; kuyachanganya kungeleta madhara makubwa mwilini. Kinyonga naye kutokana na tamaa, hakufuata maagizo. Alikula maembe, machungwa, maparachichi, tikitimaji bila kusahau tufaha. Ghafla, alianza kutetemeka na kuanguka chini. Aliposimama, mwili wake ulianza kubadilika rangi kulingana na rangi ya kile kilichokuwa karibu naye.
13. Ni ukweli kuwa kinyonga na wenzake
- Ahawakufahamu lolote kuhusu matunda
- Bwalikuwa wakiona matunda kwenye redio tu
- Chawakuwa wamewahi kula matunda
- Dhawakujua kuwa matunda yalikuwa na umuhimu
Answer
C. hawakuwa wamewahi kula matunda
Ilikuwa mara yao ya kwanza kuona matunda; walikuwa wakiyasikia redioni tu, kwa hivyo hawakuwa wamewahi kuyala.