naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 11

Madhara yaliyompata kinyonga yalitokana hasa na nini?

From Kiswahili — Monitoring Learners Progress 2025 (Set 9) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali 11-15.
Hapo zamani za kale, kinyonga hakuwa jinsi alivyo siku hizi. Alikuwa kama wanyama wengine. Hakuwa akibadilika rangi kila wakati. Siku moja, yeye na marafiki zake walialikwa katika sherehe iliyokuwa ikifanyika mjini. Yeye na wenzake waliingia katika gari na kufunga safari ya kuelekea mjini. Waliwasili mjini mwendo wa adhuhuri. Walipofika, walielekezwa mahali pa sherehe moja kwa moja. Sherehe ilipokaribia mwisho, wageni wote walielekezwa mahali pa kupata chakula. Hiyo ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa wageni waliotoka kijijini kuona matunda. Mengi walikuwa wakiyasikia tu kwenye redio na kuyaona magazetini. Kabla ya kuanza kula, walipewa onyo. Waliambiwa kuwa matunda hayo hayakuwa ya kawaida. Hakuna aliyeruhusiwa kula zaidi ya aina moja ya matunda; kuyachanganya kungeleta madhara makubwa mwilini. Kinyonga naye kutokana na tamaa, hakufuata maagizo. Alikula maembe, machungwa, maparachichi, tikitimaji bila kusahau tufaha. Ghafla, alianza kutetemeka na kuanguka chini. Aliposimama, mwili wake ulianza kubadilika rangi kulingana na rangi ya kile kilichokuwa karibu naye.

11. Madhara yaliyompata kinyonga yalitokana hasa na nini?

  1. Akutosikia
  2. Bkubadilika rangi
  3. Ctamaa
  4. Dkuwa na njaa

Answer

C. tamaa

"Kinyonga naye kutokana na tamaa, hakufuata maagizo."

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test