CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 9
Nyuki hufanya kazi hata wakati wa jua na baridi kutokana na nini?
From Kiswahili — Monitoring Learners Progress 2025 (Set 9) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 6-10.
Binadamu wana mengi wanayoweza kujifunza kutoka kwa viumbe wengine walioumbwa na Mungu. Viumbe ambao ni mfano bora kwa binadamu ni nyuki. Nyuki wanajulikana kwa mambo mawili makuu. Jambo la kwanza ni uwezo wao kuunda chakula kitamu kuliko vyote; asali. Jambo jingine ni ule uwezo wao wa kuwaangamiza watu au wanyama iwapo watamvamia kwa pamoja. Mawili hayo ni mambo wanayoweza kufanya licha ya kuwa na umbo dogo sana. Je, kwa nini mambo hayo huwezekana?
Jambo la kwanza ni kuwa nyuki huwa na bidii sana. Utawaona wakiingia na kutoka katika mzinga wao tangu asubuhi hadi jioni bila kuchoka. Wao hufanya hivyo jua liwake au pawe na baridi. Wao si kama binadamu wengine ambao wanaweza wakakataa kufanya kazi kwa kusema kuwa kuna jua, mvua au baridi kali. Binadamu wanafaa kuwa na bidii kama ya nyuki. Jambo jingine ni umoja. Nyuki huwa na ushirikiano wa hali ya juu. Wao hufanya kazi wakiwa na umoja wa hali ya juu. Umoja kama huo ukiwa miongoni mwa binadamu, tutaweza kufanya mambo makubwa sana.
9. Nyuki hufanya kazi hata wakati wa jua na baridi kutokana na nini?
- AUmoja wao
- BWingi wao
- CBidii yao
- DUdogo wao
Answer
C. Bidii yao
"nyuki huwa na bidii sana… jua liwake au pawe na baridi".
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Kifungu kinaeleza kuwa wakati wa jua, mvua na baridi kaliQuestion 10
- Madhara yaliyompata kinyonga yalitokana hasa na nini?Question 11
- Kinyonga na wenzake walikuwa wakiishi wapi?Question 12
- Ni ukweli kuwa kinyonga na wenzakeQuestion 13
- Badala ya kutumia neno kinyonga mwandishi angetumia neno lipi tena?Question 14
- Kichwa kinachofaa kwa ufahamu huu niQuestion 15