CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 13
Shairi hili ni la aina gani?
From Kiswahili — Assessment 2025 (Set 7) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ushairi
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali 11 hadi 15.
Mtoto anayo haki, ya kuishi ulimwenguni,
Asifanyiwe mkiki, kutopelekwa shuleni,
Pia asipewe mkuki, kwenda shida mwirumi,
Tumpeleke shuleni, mtoto masomo afaidike.
Mzigo haubebeki, mtoto wampa kwa nini?
Mawe hayabudiliki, wamwajiri kuyagongani?
Kutwa kucha hubanduki, wamtesa maskini,
Tumpeleke shuleni, mtoto masomo afaidike.
Kama unayo malaki, na pesa zako mfukoni,
Ama zingine kwenye benki, maelfu na mamilioni!
Saidia mahuluki, akubariki Manani!
Tumpeleke shuleni, mtoto masomo afaidike.
13. Shairi hili ni la aina gani?
- ATathlitha
- BTarbia
- CTakhmisa
- DTathnia
Answer
B. Tarbia
Kila ubeti una mishororo minne: tarbia.