CBC Grade 5 Kiswahili Mid Term 1 Exam 2025 · Question 9
Mbwa alivuka mto huku akiangalia
From Kiswahili — Midterm One Assessment 2025 (Set 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Jibu maswali baada ya kusoma kifungu hiki.
Mbwa alikuwa ameiba nyama nzuri kutoka kwa Bwana Bucha. Alitoroka kuelekea kwao. Mbwa huyo alikiuma kipande hicho cha nyama mdomoni. Alipokuwa akienda, alifika kwenye mto. Alilazimika kuuvuka mto huo ambao haukuwa na daraja kubwa la kuvukia. Mbwa alianza kupita polepole juu ya mti wa daraja ili asianguke na pia asiangushe nyama yake. Alitembea bila kuteleza huku akiangalia kwenye maji. Mara alimwona mbwa mwingine kama yeye akitembea ndani ya maji naye pia akiwa amebeba nyama mdomoni. Alitamani nyama yake akafungua mdomo ili amnyang'anye! Kwa bahati mbaya, nyama yake ilianguka majini.
9. Mbwa alivuka mto huku akiangalia
- Ajuu
- Bkwa maji
- Ckwenye maji
- Dmbele.
Answer
C. kwenye maji
"Alitembea bila kuteleza huku akiangalia kwenye maji."