CBC Grade 5 Kiswahili Mid Term 1 Exam 2025 · Question 12
Shangazi ni nani?
From Kiswahili — Midterm One Assessment 2025 (Set 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kisha ujibu swali la 11-15.
Mama alikuwa mgonjwa. Akawa amelala kitandani. Alinituma niende nimwite shangazi. Nilienda upesi sana. Shangazi alipokuja alimpikia uji akanywa. Chakula kingine alichopika, mama alikula kidogo tu. Shangazi alipoenda kuteka maji, mama alikuwa ameanza kupata nafuu.
Niligundua kuwa mtu akiwa mgonjwa anafaa awe na mtu wa kuongea naye kidogokidogo. Pia awe na mtu wa kumwangalia na kumhudumia kwa shughuli mbalimbali; akihitaji kitu chochote aletewe.
Pia mgonjwa anafaa ale na anywe. Kula kunaongeza nguvu na kumsaidia mgonjwa apone haraka. Tusiwaache wagonjwa peke yao bila kuwasaidia. Wasipohudumiwa vizuri wanaweza kuaga!
12. Shangazi ni nani?
- ADada ya mama.
- BDada ya baba.
- CMama mdogo.
- DKaka ya mama.
Answer
B. Dada ya baba.
Shangazi ni dada ya baba; dada ya mama ni mama mdogo au mama mkubwa.