naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Mid Term 1 Exam 2025 · Question 3

Nguo tunafua ilhali mwili tuna

From Kiswahili — Midterm One Assessment 2025 (Set 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kisha ujibu maswali.
Mimi ninaupenda mwili wangu. Nina kichwa, macho, pua na masikio. Aidha, nina mdomo, mikono, tumbo na miguu. Kila sehemu inanisaidia. Kichwa kina ubongo ambao husaidia kufikiria. Macho huona vitu vingi. Pua hunusa. Mdomo huzungumza na kula. Mikono hushika vitu. Masikio husikia. Tumbo hupokea chakula. Ninatembea na kukimbia kwa miguu.
Ninaupenda mwili wangu. Ninautunza vizuri. Kila siku mimi hupiga mswaki, huoga na kuzichana nywele zangu. Ninazikata kucha zangu mara kwa mara na kuvaa nguo safi zilizofuliwa kwa maji na sabuni. Sote tutunze miili yetu. Tusipoitunza, itashambuliwa na magonjwa. Hatutaweza kusoma, kucheza, kula wala kufanya kazi yoyote tukiugua.

3. Nguo tunafua ilhali mwili tuna

  1. Aoga
  2. Bosha
  3. Cnawa
  4. Dsafisha.

Answer

A. oga

Nguo hufuliwa, mwili huogeshwa: tunaoga (au tunaosha mwili).

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test