naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Mid Term 1 Exam 2025 · Question 6

Mbwa alimwibia nani nyama?

From Kiswahili — Midterm One Assessment 2025 (Set 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Jibu maswali baada ya kusoma kifungu hiki.
Mbwa alikuwa ameiba nyama nzuri kutoka kwa Bwana Bucha. Alitoroka kuelekea kwao. Mbwa huyo alikiuma kipande hicho cha nyama mdomoni. Alipokuwa akienda, alifika kwenye mto. Alilazimika kuuvuka mto huo ambao haukuwa na daraja kubwa la kuvukia. Mbwa alianza kupita polepole juu ya mti wa daraja ili asianguke na pia asiangushe nyama yake. Alitembea bila kuteleza huku akiangalia kwenye maji. Mara alimwona mbwa mwingine kama yeye akitembea ndani ya maji naye pia akiwa amebeba nyama mdomoni. Alitamani nyama yake akafungua mdomo ili amnyang'anye! Kwa bahati mbaya, nyama yake ilianguka majini.

6. Mbwa alimwibia nani nyama?

  1. AMto
  2. BMbwa mwingine
  3. CBwana Bucha
  4. DMwenye Bucha.

Answer

C. Bwana Bucha

"Mbwa alikuwa ameiba nyama nzuri kutoka kwa Bwana Bucha."

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test