CBC Grade 5 Kiswahili Mid Term 1 Exam 2025 · Question 2
Mtu akitaka kuhisi ladha ya kitu atatumia
From Kiswahili — Midterm One Assessment 2025 (Set 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kisha ujibu maswali.
Mimi ninaupenda mwili wangu. Nina kichwa, macho, pua na masikio. Aidha, nina mdomo, mikono, tumbo na miguu. Kila sehemu inanisaidia. Kichwa kina ubongo ambao husaidia kufikiria. Macho huona vitu vingi. Pua hunusa. Mdomo huzungumza na kula. Mikono hushika vitu. Masikio husikia. Tumbo hupokea chakula. Ninatembea na kukimbia kwa miguu.
Ninaupenda mwili wangu. Ninautunza vizuri. Kila siku mimi hupiga mswaki, huoga na kuzichana nywele zangu. Ninazikata kucha zangu mara kwa mara na kuvaa nguo safi zilizofuliwa kwa maji na sabuni. Sote tutunze miili yetu. Tusipoitunza, itashambuliwa na magonjwa. Hatutaweza kusoma, kucheza, kula wala kufanya kazi yoyote tukiugua.
2. Mtu akitaka kuhisi ladha ya kitu atatumia
- Aulimi
- Bmasikio
- Cpua
- Dmiguu.
Answer
A. ulimi
Ladha huhisiwa kwa ulimi.